AINA 10 ZA WANANDOA BABU ANAFAFANUA



1. KUMBIKUMBI

Hawa huongozana kila mahali. Yaani wanapendana hadi mahasidi wanatamani wanywe maji ya betri. 


2. WAPAMBANAO

Hawa muda wote hupambana , hubishana na kurushiana maneno  na kukosoana utasema wanaachana kesho ila huwa wanapendana , hawaachani ng'o. 


3.WAZAZI WENZA

Hawa kwa asilimia kubwa huwa wapo kwa ajili ya watoto au wapo kufurahisha ndugu na wazazi.  Moyoni walishaachana ila nje wanaonekana pamoja kusogeza siku watoto wakue. 


4. WASITAO

Hawa ni kama hawana uhakika na ndoa yao na hawapendi kabisa kujulikana kama ni mke na mume labda ikilazimu sana. Wanaweza kuwa na miaka mingi kwenye ndoa ila wanaishi kama bado wanachunguzana.


5.VING'ANG'ANIZI

Wanajijua kabisa hawapendani ila wanatumia nguvu nyingi kuhakikisha wanaendelea kuwa pamoja kwani kila mmoja yupo kwenye ndoa kimkakati na kimaslahi. Hawa huwa  hawaamini kama kuna upendo wa kweli na kama watu wanaweza kuishi kama marafiki. Wakiona watu wanapendana wanahisi kuna limbwata limetumika na wao wenyewe wanakuwaga washirikina. 


6. WAIGIZAJI

Hawa huwa maadui wakubwa wawapo nyumbani lakini wakiwa mbele za watu hujifanya wanapendana. 


7. UPANDE MMOJA

Hawa unakuta mmoja ndiye anaendesha ndoa kwa kila kila jambo yeye ndiye anaamua kila kitu na mwenzake hukaa tu kama msukule na kukubaliana na kila lisemwalo ili kuepusha shari japo moyoni huwa hampendi wala kumkubali mwenzi wake. 


8.WANAHURIA

Yaani kila mtu anaishi kivyake ni kupeana tu taarifa leo nasafiri au jana nimenunua kiwanja yaani ni taarifa tu . Kila mtu ana mapato yake na matumizi yake na hakuna mipango ya pamoja. 


9. WACHAMUNGU

Hawa wana hofu ya Mungu. Wanaishi kwa malengo na wanamtegemea Mungu na kufanya maombi pamoja na maamuzi yote yanatokana na imani yao. 

 

10. WADAU

Hawa huishi kama wadau wa kibiashara na ndoa huendeshwa kama taasisi au mradi fulani. Mambo yanaenda kwa mpangilio, heshima ipo, maendeleo yapo ila ndoa haina mashamsham wala upendo kila mtu ana siri zake moyoni na mambo yake ya kisirisiri.


#hdmasterplan

#wenyeweclassicgroup

#kitambo_kidogo_wcg

#wenyeweclassicgroup_2015

#wenyewe_classic_updates_from

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI