Kuna hali inazidi kushika kasi miongoni mwa wanaume wa kizazi hiki. Unakuta kijana anaonekana yupo sawa, ana tabasamu, ana marafiki, ana gari au hata ndoa lakini ndani yake kuna kilio kisichosikika, kuna mzigo Mkubwa usiobebeka, kuna uchovu wa kuishi maisha yasiyo yake. Mwanaume wa sasa amekuwa kama mchezaji wa maigizo. Anaigiza mafanikio, anaigiza furaha, anaigiza mapenzi yote ili aonekane yupo juu, awe na heshima mbele ya marafiki, aonekane “mwanaume wa maana” mbele ya jamii. Lakini ni wangapi wameangamia kwa sababu hiyo? Mashinikizo ya watu yamemweka mwanaume kwenye kona mbaya sana. Mwanaume anahisi hawezi kulalamika, hawezi kuomba msaada, hawezi kuanguka. Akilia anaitwa muoga. Akishindwa anaitwa dhaifu. Matokeo yake, anapigana na maisha peke yake mpaka anapotea kimya kimya. Depresheni inamla ndani kwa ndani, na hakuna anayejua. Leo hii kijana anaoa si kwa sababu ya upendo, bali kutimiza matarajio ya watu,jamii,washikaji,na marafiki. Anatafuta mwanamke “...
Comments