Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
WASIFU WA MKOA
Utangulizi
Mkoa wa Geita una eneo la kilometa za
mraba 21,879 (Geita 6,375 km2, Bukombe 6,798 km2, Chato 3,572 km2, Mbogwe 3,684
km2, na Nyang`hwale 1,450 km2), kati ya hizo kilomita za mraba 19,933 ni za
nchi kavu na kilomita za mraba 1,946 ni za maji. Mkoa una Wilaya tano (5),
Majimbo tisa (9) ya uchaguzi, Halmashauri sita (6), Miji midogo 2, Tarafa 20,
Kata 122, Vijiji 486, Vitongoji 2,195 na Mitaa 65. Wilaya hizo ni Geita,
Nyang’hwale, Chato, Bukombe na Mbogwe. Mkoa unajumuisha Halmashauri ya Manispaa
ya Geita, Halmashauri za Wilaya za
Geita, Nyang’hwale, Chato, Bukombe na Mbogwe. Kwa mujibu wa
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Geita una wakazi wapatao
2,977,608 ambapo Wanaume ni 1,463,764 na Wanawake ni 1,513,844.
Hali ya
Uchumi.
Hali ya Uchumi ya Mkoa imeendelea
kuimarika ambapo Pato halisi lilikua kutoka Shilingi 7,031,590,000/= mwaka 2021 hadi Shilingi 9,122,637,000/= mwaka 2024 sawa na ukuaji wa asilimia 31
Vilevile, pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi 2,769,308/= mwaka 2021 hadi shilingi 2,814,714/= mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 1.6.
Ulinzi na Usalama
Hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa imeendelea kuwa shwari
kutokana na ushirikiano uliopo baina ya vyombo vya Dola na Wananchi.
Hali hii imewawezesha wananchi kuishi kwa amani na utulivu na kuendelea na
shughuli zao za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
MAFANIKIO
YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA MKOA WA GEITA
Mkoa wa Geita umepata mafanikio makubwa
katika nyanja na sekta zote. Mafanikio hayo yametokana na uimara wa Chama cha
CCM katika kuendelea kuisimamia Serikali kwa lengo la kuhakikisha inatekeleza
na kutoa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Kutokana na hilo, kwa kipindi cha kuanzia
machi 2021 – Juni, 2025, Mkoa umepokea Shilingi trilioni 1,442,899,340,734/=
kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika sekta za afya, elimu,
miundombinu ya usafiri na usafirishaji, maji, nishati, kilimo, mifugo, uvuvi,
misitu, utalii, viwanda, biashara, uwezeshaji wananchi kiuchumi na miradi ya
kimkakati. Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi husika ni kama
ifuatavyo:
Huduma za Jamii
Afya
Mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya kutolea huduma za
afya, kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi na
kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi. Mafanikio hayo
ni pamoja na:
(a)
Kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali za Halmashauri
za Bukombe, Chato, Geita, Geita Manispaa, Mbogwe na Nyang’hwale;
(b)
Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la
wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Halmashauri ya Geita (Nzera) na ukarabati
wa Hospitari ya Halmashauri ya Bukombe na
Manispaa ya Geita;
(c)
Kuongezeka kwa idadi ya zahanati kutoka
129 mwaka 2021 hadi 198 mwaka 2025;
(d)
Kuongezeka kwa vituo vya afya kutoka 25
mwaka 2021 hadi 42 mwaka 2025;
(e)
Kuongezeka kwa nyumba za watumishi wa
afya kutoka 180 mwaka 2021 hadi 230 mwaka 2025;
(f)
Kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa,
vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya
kutoka asilimia 80 mwaka 2021 hadi asilimia 90 mwaka 2025;
(g)
Kupunguza vifo vya mama wajawazito
kutoka 57 mwaka 2021 hadi vifo 55 mwaka 2025; na
(h)
Kupunguza maambukizi ya Virusi vya
UKIMWI kutoka 5.1% mwaka 2021 hadi kufikia 4.90% mwaka 2025.
Elimu
Mafanikio
yaliyopatikana katika sekta ya elimu yamewezesha kuongezeka kwa uandikishaji na
udahili wa wanafunzi, ufaulu pamoja na kupunguza umbali wa wanafunzi kufuata
huduma ya elimu. Mafanikio hayo ni pamoja na:
(a) Kuendelea kutekeleza Mpango wa Elimu bila Ada kuanzia elimu ya awali hadi
kidato cha sita kwa kuongeza fedha za kugharamia mpango huo kutoka Shilingi
6,486,387,724.00/= mwaka 2021 hadi Shilingi 19,989,544,192/=mwaka 2025;
(b) Kuongezeka kwa idadi ya shule za msingi na Awali kutoka 641 mwaka 2021
hadi 792 mwaka 2025;
(c) Kuongezeka kwa idadi ya shule za sekondari kutoka 130 mwaka 2021 hadi 240
mwaka 2025;
(d) Kuongezeka kwa idadi ya vyumba vya madarasa ya shule za msingi na
sekondari kutoka madarasa 7,206 mwaka 2021 hadi 10,540 mwaka 2025;
(e) Kuongezeka kwa nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka
2,272 mwaka 2021 hadi 2,375 mwaka 2025;
(b)
Kuimarika kwa ufaulu kwa wanafunzi wa
darasa la saba kwa asilimia 82.49 mwaka 2021 na asilimia 71.53 mwaka 2024,
kidato cha nne asilimia 84.56 mwaka 2021 na asilimia 94.45 mwaka 2024 na kidato
cha sita kwa asilimia 99.98 mwaka 2021 na asilimia 99.96 mwaka 2024;
(c)
Idadi ya walimu katika ngazi ya elimu ya
msingi imeongezeka kutoka 8,876 mwaka 2021 hadi 9,156 mwaka 2025 na elimu sekondari
kutoka walimu 3,398 mwaka 2021 hadi 3,696 mwaka 2025;
(d)
Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya
vyuo vya kati (VETA) kutoka chuo kimoja mwaka 2021 hadi vyuo 05 mwaka 2025, vyumba
vya maabara kutoka 165 mwaka 2021 hadi 338 mwaka 2025. Aidha, mabweni ya wasichana
74 katika shule za sekondari, mabwalo 19 na hosteli 5; majengo ya utawala 12,
matundu ya vyoo 14,133, yamejengwa na kukamilika;
(e)
Kuongezeka kwa Wanafunzi wa MEMKWA
walioandikishwa kutoka 2,169 mwaka 2021 hadi wanafunzi 2,269 mwaka 2025; na
(f)
Kuongezeka kwa Wanafunzi wenye mahitaji
Maalum kwa shule za msingi na sekondari kutoka wanafunzi 1,052 mwaka 2021 hadi
wanafunzi 2,233 mwaka 2025.
Maji
Katika kipindi cha kuanzia
mwaka 2021 hadi 2025 Serikali ya awamu ya sita iliweka kipaumbele cha kuendelea
kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kaya nyingi zaidi zinaunganishwa na huduma ya maji. Katika
kutekeleza azma hiyo mafanikio makubwa yamepatikana Mkoani Geita kama ifuatavyo:
(a)
Kuimarika kwa huduma ya upatikanaji wa
maji safi kwa wananchi wa Mkoa kutoka 65% mjini na 61% vijijini mwaka 2021 hadi
asilimia 75% mjini na 65% vijijini mwaka 2025;
(b)
Kuongezeka kwa uzalishaji wa maji katika
Mji wa Geita kutoka lita milioni 5,200,000 kwa siku mwaka 2021 hadi 6,800,000
kwa siku mwaka 2025;
(c)
Kuongezeka
kwa idadi ya vijiji vyenye huduma ya maji kutoka Vijiji 204 mwaka 2021 hadi Vijiji 420 mwaka 2025;
(d)
Kukamilika kwa miradi 81 na kuanza kutoa
huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini na kuendelea na utekelezaji wa
miradi 20 iliyofikia wastani wa asilimia 51 chini ya usimamizi wa RUWASA; na
kukamilika kwa miradi 3 ya maji na kuendelea kutekeleza miradi 4 iliyofikia
wastani wa asilimia 60 chini ya usimamizi wa GEUWASA; na
(e)
Kuongezeka kwa kasi ya uchimbaji wa
visima vya maji kutoka visima 299 mwaka
2021 hadi visima 389 mwaka 2025;
Aidha chini ya usimamizi wa
GEUWASA imetekelezwa miradi ifuatayo:-
b) Ujenzi
wa mradi wa maji Bung'wangoko utakaohudumia wakazi 6,200 katika vijiji vya
Chabulongo, Bung'wangoko center na Mshinde;
c) Utanuzi
wa Chujio la maji (Treatment Plant) Nyankanga;
d) Ujenzi
wa mradi wa maji Mbogwe - Msumbwe utakaohudumia wakazi 7,200 katika maeneo ya
Kagri, Masumbwe na Nyakafuru;
e) Utanuzi
wa mtandao wa maji kata ya Mbogwe na Iponya utakaohudumia vijiji vya
Bwendanseko, Nyambubi, Buluhe na Nyashimba;
f) Ujenzi
wa mradi wa maji katoro - Buseresere ambao umekamilika na unahudumia wakazi wa
Katoro, Ludete Nyamigota na Buseresere. Mradi umesanifiwa kuhudumumia wakazi
68,000; na
g) Ujenzi
wa mradi wa maji kutoka Ziwa Viktoria - Miji 28 utakahudumia kata 13 za Mji wa
Geita na vijiji 19 vya Geita DC ambayo vinapitiwa na mradi. Aidha utekekelezaji
wake unandelea.
Sekta za Uzalishaji
Kilimo
Serikali ya awamu ya
sita imeendelea kutekeleza shughuli za
kilimo katika Mkoa wa Geita kwa kuhakikisha kilimo kinakuwa chenye tija na
usalama wa chakula unaimarika. Katika kusimamia hilo mafanikio mbalimbali
yamepatikana ikiwemo:
(a)
Kuanzishwa kwa skimu za umwagiliaji na kufikia skimu 02
mwaka 2025;
(b)
Kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa
mbolea ya ruzuku kutoka tani 1,684.67 mwaka 2021 hadi tani 5,934.05 mwaka 2025;
(c)
Kuimarisha huduma za ugani kwa kununua
vitendea kazi ikiwemo pikipiki 153 vipima udongo 5 na vishikwambi 175 kwa ajili
ya maafisa ugani;
(d)
Kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya
chakula kutoka tani 1,445,814 mwaka 2021 hadi tani 1,512,761mwaka 2025 na mazao
ya biashara kutoka tani 67736 mwaka 2021 hadi tani 72820 mwaka 2025;
(e)
Kuimarisha ushiriki wa vijana katika
kilimo kwa kutoa mafunzo na ujenzi wa vitalu nyumba kwa vijana 600 mwaka 2021
na Vijana 662 kwa mwaka 2025;
(f)
Kuongezeka kwa vyama vya ushirika kutoka
512 na wanachama 44,375 mwaka 2021 hadi vyama vya ushirika 600 na wanachama
49,875 mwaka 2025;
(g)
Kuongeza uzalishaji wa zao la pamba
kutoka tani 9,309 mwaka 2021 hadi tani 19,632 mwaka 2025; na
Mifugo
Serikali ya awamu ya
sita chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi inatambua umuhimu wa sekta ndogo
ya Mifugo kama shughuli kuu ya kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa. Kutokana na umuhimu
huo, Serikali ya Mkoa wa Geita katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 had 2025 imeendelea
kuhimiza ufugaji wa kisasa wenye kuzingatia kinga, tiba na utafiti wa mifugo
ili ufugaji uweze kuwanufaisha wananchi. Mafanikio yaliyopatikana ni ka
ifuatavyo:-
(a)
Kusambaza dawa za ruzuku za kuogeshea
mifugo lita 839 na dozi 770,000 za chanjo ya kudhibiti ugonjwa wa homa ya
mapafu ya ng’ombe (CBPP);
(b)
Kukamilika kwa ujenzi wa jumla ya
majosho 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Geita, Geita Manispaa, Mbogwe
na Nyang’hwale kwa ajili ya kuogesha mifugo;
(c)
Kuimarisha huduma za ugani kwa kugawa
pikipiki 43 kwa maafisa mifugo;
(d)
Kuanzisha mashamba darasa ya malisho ya
mifugo yapatayo hekta 64 sawa na ekari 160;
(e)
Kutoa elimu ya ufugaji bora na
uboreshaji wa mbari za mifugo kwa kusambaza mbegu bora za mifugo zipatazo 2,000
kwa njia ya uhimilishaji;
(b)
Kuongezeka kwa uzalishaji wa nyama
kutoka tani 4,626,375 mwaka 2021 hadi tani 7,710,625 Mwaka 2025;
Uvuvi
Kwa
kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025 Mkoa umetekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ilani
ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020-2025 sura ya pili ibara ya 43 kifungu
kidogo cha (h na o). Mkoa umeimarisha vikundi vya vyama vya ushirika na kwa
lengo la kupata mitaji na hivyo kuongeza tija katika shughuli za uvuvi.
a)
Idadi ya wavuvi imeongezeka
kutoka 7,549 mwaka 2021 hadi 10,001 mwaka 2025; na
b)
Idadi ya vyombo vya uvuvi
imeongezeka kutoka 997 mwaka 2021 hadi 2,500 mwaka 2025
Shughuli
za Ufugaji samaki
Mkoa umeimarisha vikundi vya ufugaji samaki na
kituo cha kuendeleza ukuzaji viumbe maji cha Lubambangwe kwa lengo la kukuza
sekta ya ufugaji samaki.
a)
Idadi ya vizimba vya
kufugia Samaki imeongezeka kutoka 4 mwaka 2021 hadi vizimba 27 mwaka 2025; na
Madini
Serikali ya awamu ya
sita inatambua kuwa sekta ya madini ina nafasi ya kipekee katika kuchangia
ukuaji wa Pato la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni na ukuaji wa uchumi kwa
ujumla. Kwa Mkoa wa Geita, Mafanikio yaliyopatikana kutokana na sekta ya madini
ni kama ifuatavyo:-
(a)
Kuongezeka kwa uzalishaji wa madini
kutoka tani 18.21 mwaka 2021 hadi tani 27.43
mwaka 2025;
(b)
Kuongezeka kwa fedha za kigeni
zilizotokana na uuzaji wa madini kutoka Dola za Marekani 72,878,325.91 mwaka
2021 hadi Dola za Marekani 92,204,527.35 mwaka 2025;
(c)
Kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri
yatokanayo na uchimbaji wa madini kutoka Shilingi 6,163,170,093.30 mwaka 2021 hadi
Shilingi 10,582,192,189.88 mwaka 2025;
(d)
Kuongezeka kwa masoko ya madini kutoka
masoko 10 mwaka 2021 hadi masoko 20 mwaka 2025; na
(e)
Kuongezeka kwa utoaji wa leseni kwa
wachimbaji wadogo kutoka leseni 903
mwaka 2021 hadi 9,774 mwaka 2025.
Viwanda na Biashara
Kwa kipindi cha
uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mafanikio yaliyopatikana katika skta hii ni
pamoja na:
(a)
Kuongezeka kwa viwanda kutoka 824 mwaka
2021 hadi viwanda 1,542 mwaka 2025;
(b)
Kuongezeka kwa ajira za viwandani,
kutoka ajira 927 mwaka 2021 hadi ajira 15,161 mwaka 2025; na
(c)
Kuongezeka kwa utoaji wa leseni kwa
wafanya biashara kutoka leseni 1,346 mwaka 2021 hadi leseni 2,815 mwaka 2025.
Sekta ya Miundombinu
Katika kipindi cha
kuanzia mwaka 2021 hadi 2025 Serikali imendelea na ujenzi wa miundombinu
mbalimbali ikiwemo barabara, madaraja na makalvati ili kuimarisha shughuli za
kiuchumi na kijamii. Mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na:
(a)
Kuongezeka kwa mtandao wa barabara za
lami kutoka kilomita 450.86 mwaka 2021 hadi kilomita 476.87 mwaka 2025;
(b)
Kuongezeka kwa mtandao wa barabara za
changarawe kutoka kilomita 1,984.18 mwaka 2021 hadi 3,078.48 mwaka 2025;
(b)
Kukamilisha ujenzi wa makalavati 3,444
katika Wilaya za Geita, Bukombe, Chato, Mbogwe na Nyang’hwale;
(c)
Kusimika taa za barabarani kutoka taa
589 mwaka 2021 hadi taa 323 mwaka 2025;
(d)
Kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja cha
ndege cha Geita kilichopo Wilaya ya Chato;
(e)
Kukamilisha ujenzi wa madaraja 6 katika
Wilaya za Geita na Chato;
(f)
Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa
TACTIC katika Manispaa ya Geita unaohusu uboreshaji wa barabara ya urefu wa km
17 kwa kiwango cha lami;
Sekta ya Nishati
Sekta ya nishati imeendelea kuwa mhimili
muhimu katika kuwezesha utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika
Mkoa wa Geita. Kutokana na hilo, CCM iliisimamia Serikali katika kuhakikisha
kuwa Mkoa unakuwa na nishati ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi na
kijamii. Mafanikio yaliyopatikan ni pamoja na:
(a)
Kuunganisha umeme kutoka
vijiji 386 mwaka 2021 hadi vijiji 483 mwaka 2025. Aidha, mradi huu wa umeme
umeweza kuunganisha umeme katika vitongoji 1,021 kati ya vitongoji 2,195 sawa
na asilimia 46.5;
(b)
Kuendelea na utekelezaji wa
mkakati wa nishati safi ya kupikia ambao umelenga kuboresha afya ya jamii na
kulinda mazingira safi ya kupikia kwa kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi
ya kupikia na kugawa mitungi 16,275 ya gesi kwa mamalishe/wananchi;
(c)
Kukamilika kwa mradi wa
kusambaza umeme vijijini (REA3R2) ambao ulipeleka umeme katika vijiji 127 `na vitongoji
50;
(d)
Kukamilika kwa mradi wa
kusambaza umeme maeneo yaliyo pembezoni mwa miji (Peri urban ) ambao
ulifanikiwa kusambaza umeme katika mitaa
na vitongoji 45 vilivyo pembezoni mwa Manispaa
ya Geita;
(e)
Kufanikisha maboresho ya miundombinu ya usambazaji umeme
katika wilaya zote za mkoa wa Geita kwa kuondoa nguzo za miti na kuweka za zege
ambazo zinadumu kwa muda mrefu zaidi;
(f)
Kujenga njia za kusambaza
umeme katika maeneo 52 ya wachimbaji madini wadogo wa Mkoa wa Geita na hivyo
kuwapunguzia gharama za uendeshaji katika machimbo yao kwani awali walitumia
gharama kubwa katika kununua mafuta;
Sekta ya Maliasili na Utalii
Serikali ya awamu ya
sita inatambua kuwa sekta ya utalii ina umuhimu katika ukuaji wa uchumi na
maendeleo kwa ujumla. Katika kipindi cha mwaka 2021 - 2025 Mafanikio
yaliyopatikana kutokana na ekta hii ni pamoja na:
(a)
Kuweka mazingira wezeshi na kuboresha
miundombinu ya utalii;
(b)
Kubuni na kuanzisha vivutio vya utalii
ikiwemo hifadhi ya Burigi-Chato;
(c)
Kusimamia rasilimali za misitu na nyuki
minzinga 426,483.
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Serikali imeendelea
kutilia mkazo umuhimu wa maendeleo ya wananchi pamoja na ushirikishwaji wa
makundi maalum ikiwemo vijana, wanawake na Watu Wenye Ulemavu ili kuleta usawa
wa kijamii na kiuchumi kwa wote. Katika kufikia azma hiyo mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na:
(a)
Kuongezeka kwa utoaji wa mikopo ya
asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na Watu Wenye Ulemavu kutoka
Shilingi bilioni 4,936,939,735.70 mwaka 2021 hadi Shilingi bilioni
8,659,406.081.40 za mwaka 2025; na
(a) kutekeleza miradi ya miundombinu 353 ya elimu, afya na barabara pamoja na kuwezesha walengwa kujiongezea kipato kupitia ufugaji na kilimo.
Michezo na Sanaa
Serikali inatambua kuwa sekta ya michezo na sanaa ina umuhimu mkubwa katika kutoa burudani, kuelimisha jamii, kuimarisha
afya, kuunganisha jamii, kuzalisha ajira na kudumisha mila, tamaduni na
desturi za kitanzania. Mkoa umeweza kuboresha
miundombinu ya michezo na sanaa kwa lengo la kuimarisha udugu na umoja. Mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na:
(a)
Ujenzi wa viwanja vipya 2 vya mpira wa
miguu ambavyo utekelezaji wake unaendelea; na
(b)
Kuhamasisha uanzishwaji wa vilabu vya
michezo (ikiwemo Jogging).
Miradi ya Kimkakati
Serikali ya awamu ya
sita imeendelea na kutekeleza miradi ya kimkakati kwa lengo la kuongeza mapato
na kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja
na:
(a)
Kuendelea na ujenzi wa soko la samaki
katika Halmashauri ya Chato;
(b)
Ujenzi wa miundombinu ya stendi ya mabasi Chato yenye gharama ya
shilingi bilioni 14 pamoja na stendi ya Bwanga;
(b)
Kukamilika kwa machinjio ya kisasa
katika eneo la mpomvu Manispaa ya Geita;
(c)
Ujenzi wa soko la machinga-Katoro;
(d)
Kusimamia ujenzi wa mradi wa bomba la
mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); na
(e)
Kuendelea na ujenzi wa uwanja wa mpira
wa magogo katika Manispaa ya Geita wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000
kwa gharama ya shilingi bilioni 2.1.
Utawala
bora
Serikali ya awamu ya
sita imejipambanua katika ujenzi wa demokrasia, utawala bora na utawala wa
sheria ili kuwa na mazingira wezeshi kwa ajili ya ustawi wa jamii na maendeleo.
Kuimarika kwa utawala bora kumewezesha kukuza demokrasia, kujenga moyo wa
uzalendo, kudumisha amani na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:
(a)
Kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama
ikiwemo Mahakama za Wilaya ambapo mwaka 2021 kulikuwa na Mahakama 28 lakini
hadi 2025 Mahakama zimeongezeka hadi 31;
(b)
Kuongezeka kwa vituo vya polisi kutoka
33 mwaka 2021 hadi vituo 38 mwaka 2025; na
HITIMISHO
Serikali ya awamu
ya sita katika Mkoa wa Geita imejipanga kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) ya mwaka 2025-2030 ili kufikia maleng ya Chama ya kuwahudumia wananchi
katika nyanja zote za maisha.
Comments