MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA KATIKA MKOA WA SHINYANGA KATIKA KIPINDI CHA SERIKALI YA AWAMU YA SITA
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Niliyesimama Mbele yenu naitwa Mboni Mohamed Mhita. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa Kuniteua na kunipa jukumu la ukuu wa Mkoa kwa Mkoa wa Shinyanga. Namuahidi kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, na Uzalendo.
Niko Mbele yenu ili kuzungumzia mafanikio makubwa ambayo Mkoa wa Shinyanga umepata katika awamu hii ya Sita, inayo ongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Na kwa namna ya kipekee, Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa Uongozi wake Thabiti ambao umepelekea Mkoa wa Shinyanga kunufaika na kufaidika katika awamu hii ya sita.
Najua mna shauku ya kujua mambo hayo. Nami nitaanza, kwa kuwaelezea kuhusu Mkoa wa Shinyanga, Miradi ya Maendeleo, Uwekezaji kwenye Miradi ya Kimkakati na namna ambayo tumejikita kuwainua Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kiuchumi.
Ndugu Waandishi wa Habari;
Nipongeze sana utaratibu huu uliowekwa na Wizara ya Habari, sanaa, utamaduni na Michezo ambao unatuma fursa ya kuainisha mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya sita inayo ongozwa na Kiongozi wetu,
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mikoa yetu.
1.0 WASIFU WA MKOA WA MKOA WA SHINYANGA
i. Mkoa wa Shinyanga una ukubwa wa kilometa za mraba 18,557
ii. Mkoa una jumla ya watu 2,241,299 ambapo kati ya hao Wanaume ni 1,102,879 na Wanawake ni 1,138,420.
iii. Kiutawala Mkoa una Wilaya tatu ambazo ni Shinyanga, Kahama na Kishapu; Halmashauri Sita (Halmashauri mbili za Manispaa - Shinyanga na Kahama; na Halmashauri nne za Wilaya - Kishapu, Shinyanga, Msalala na Ushetu); Majimbo ya Uchaguzi saba (Shinyanga Mjini, Solwa, Itwangi, Kahama, Msalala, Ushetu na Kishapu), Tarafa 14, Kata 130 vijiji 506, Mitaa 90 na Vitongoji 2,704.
iv. Kikubwa zaidi ni kuwa wana Shinyanga ni watu wakarimu.
2.0 MAFANIKIO YA MKOA KISEKTA
Ndugu Waandishi wa Habari;
Kama tujuavyo Serikali ya awamu ya Sita (6) imejikita kwenye kuboresha kila sekta. Katika kipindi cha awamu ya sita, Mkoa wa Shinyanga umepokea Shilingi trilioni 1.563 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika sekta za afya, elimu, miundombinu ya usafiri na usafirishaji, maji, nishati, madini, kilimo, mifugo, viwanda, biashara, uwezeshaji wananchi kiuchumi na miradi ya kimkakati.
Tumesikia jinsi kiongozi wetu Mkuu, Mheshimiwa Rais akisisitiza ukusanyaji wa mapato. Mkoa wa Shinyanga unafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, na hii nikutokana na utoaji wa Elimu kwa wananchi.
3
Kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2020/21 hadi Machi, 2025, Mkoa wa Shinyanga uliidhinishiwa kukusanya mapato ya ndani ya jumla ya Shilingi bilioni 151.87 kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hadi kufikia Machi, 2025, jumla ya Shilingi bilioni 150.26 zilikusanywa, sawa na asilimia 98. Fedha hizi zilikusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama Fedha za Uwajibikaji wa Taasisi kwa Jamii yani CSR (Hatukuishia kwenye local content); Ushuru wa mazao na mifugo; pamoja na Ada mbalimbali zinazotozwa na Halmashauri mfano ada za leseni za biashara na mirabaha katika Sekta ya madini.
Katika fedha hizo Miradi yenye thamani ya Tsh. bilioni 65.5 ilitekelezwa kupitia fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu na Ukamilishaji wa Maboma ya katika Sekta za Elimu na Afya; ikiwemo Ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi na Watoto Hospitali ya Manispaa Kahama lenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Katika kipindi cha miaka minne (Machi 2021 hadi Aprili 2025), Mikoa ya Kimadini ya Shinyanga na Kahama imekusanya mapato ya jumla ya Shilingi bilioni 540.17. Aidha, kwa mwaka 2024/2025 hadi kufikia Aprili 2025 kiasi cha Shilingi bilioni 131.51 kimekusanywa ikilinganishwa na lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 165 sawa na asilimia 79.70. (Elimu)
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yenye Mikoa ya kikodi Shinyanga na Kahama kwa kipindi cha miaka minne (Machi 2021 hadi Machi 2025) imekusanya mapato ya Shilingi bilioni 202.54 kati ya lengo la Shilingi bilioni 199 sawa na asilimia 102%. (Elimu)
4
2.1 Huduma za Jamii
2.1.1 Sekta ya Afya
Mkoa umepokea shilingi bilioni 79.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za Afya.
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya kutolea huduma za afya, kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi. Mafanikio mengine ni pamoja na:
(a) Kukamilishwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mwawaza
(b) Kuongezeka kwa idadi ya Hospitali za Wilaya 5 kutoka mbili mwaka 2020 hadi Saba mwaka 2025 katika Halmashauri za Shinyanga DC, Msalala DC, Ushetu DC, Shinyanga MC na Kishapu DC (Hospitali ya Mwadui)
(c) Kuongezeka kwa vituo vya afya 13 kutoka 25 mwaka 2020 hadi 38 mwaka 2025 vya Kambarage & Ihapa (Shinyanga MC), Bulige & Mwalugulu (Msalala DC) Lyabukande, Mwakitolyo & Salawe (Shinyanga DC), Ng’wanhalanga & Lagana (Kishapu DC), Igwamanoni, Ulowa & Nyalwelwe (Ushetu DC), Kinaga (Kahama MC)
(d) Kuongezeka kwa idadi ya zahanati 51 kutoka 226 mwaka 2020 hadi 277 mwaka 2025;
(e) Kuongezeka kwa nyumba 5 za watumishi wa afya kutoka 198 mwaka 2020 hadi 203 mwaka 2025 katika vituo vya Nyalwelwe, Chambo, Butibu (Ushetu DC), Msalala DH (Msalala DC) na;
5
(f) Kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoka asilimia 76 mwaka 2020 hadi asilimia 88 mwaka 2025.
(g) Kuongezeka kwa Watumishi 2,104 wa Kada ya Afya 708 kutoka 2,104 awali na kuwa 2,812.
(h) Kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025 Jumla ya Majengo ya Wagonjwa wa nje (OPD) katika zahanati 21 na majengo ya Mionzi, Jengo la kuhifadhia maiti katika vituo vya afya 2 yamejengwa; pamoja na kujenga chuo cha Afya cha Ntobo kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kupitia Fedha za Uwajibikaji wa Taasisi kwa Jamii yani CSR.
2.1.2 Elimu
Mkoa umepokea shilingi bilioni 155.24 kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu na kuongeza idadi ya walimu kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya kati.
Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu yamewezesha kuongezeka kwa uandikishaji na udahili wa wanafunzi, ufaulu pamoja na kupunguza umbali wa wanafunzi kufuata huduma ya elimu. Mafanikio mengine ni pamoja na:
(a) Kuongezeka kwa idadi ya shule za msingi 29 kutoka 682 mwaka 2020 hadi 711 mwaka 2025;
(b) Kuongezeka kwa idadi ya shule za sekondari 14 kutoka 186 mwaka 2020 hadi 200 mwaka 2025;
(c) Kuongezeka kwa idadi ya vyumba vya madarasa 946 ya shule za msingi kutoka madarasa 4,940 mwaka 2020 hadi 5,886
6
mwaka 2025 na vyumba vya madarasa 1,282 ya shule za sekondari kutoka 1,583 mwaka 2020 hadi madarasa 2,865 mwaka 2025;
(d) Kuongezeka kwa idadi ya Madawati 35,919 kutoka 104,581 mwaka 2020 hadi Madawati 140,500 kwa mwaka 2025;
(e) Kuongezeka kwa Viti na Meza 38,789 kutoka 63,024 mwaka 2020 hadi Madawati 101,813 kwa mwaka 2025;
(f) Kuongezeka kwa Vyumba vya Maabara 118 kutoka 220 mwaka 2020 hadi 338 mwaka 2025;
(g) Kuongezeka kwa Idadi ya mabweni 53 kutoka 78 mwaka 2020 hadi mabweni 131 mwaka 2025;
(h) Kuongezeka kwa maktaba 22 kutoka 9 mwaka 2020 hadi 31 mwaka 2025;
(i) Kuongezeka kwa nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari 209 kutoka 1,617 mwaka 2020 hadi 1,826 mwaka 2025;
(j) Kuongezeka kwa idadi ya walimu walioajiriwa 1,215 katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari kutoka walimu 6,412 mwaka 2020 hadi walimu 7,627 mwaka 2025; na
(k) Kuongezeka kwa ujenzi wa vyuo vya kati 2 kutoka chuo kimoja hadi vyuo vitatu mwaka 2025.
(l) Kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025 Jumla ya madarasa 43 zimejengwa kupitia Fedha za Uwajibikaji wa Taasisi kwa Jamii yani CSR kwa shule za msingi.
(m) Kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025 Jumla ya madarasa 58, viti na meza 4813 vimetengenezwa kupitia Fedha za Uwajibikaji
7
wa Taasisi kwa Jamii yani CSR kwa shule za Sekondari pamoja na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA - Bugarama
2.1.3 Maji
Mkoa umepokea kiasi cha shilingi bilioni 113.33 katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 kwa ajili ya huduma ya maji. Mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na:
(a) Kuimarika kwa huduma ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi wa Mkoa kutoka asilimia 63 mwaka 2020 hadi asilimia 79 mwaka 2025 maeneo ya mijini na asilimia 51 mwaka 2020 hadi asilimia 68 mwaka 2025 vijijini;
(b) Kuongezeka kwa idadi ya vijiji 222 vyenye huduma ya maji kutoka Vijiji 162 mwaka 2020 hadi Vijiji 384 mwaka 2025;
(c) Kukamilika kwa miradi 64 na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini na kuendelea na utekelezaji wa miradi 75 iliyofikia wastani wa asilimia 62;
(d) Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria katika Vijiji 111 katika maeneo ya Kishapu, Shinyanga na Kahama;
2.2 Sekta za Uzalishaji
2.2.1 Kilimo
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na
(a) Kuongezeka kwa skimu 13 za umwagiliaji kutoka skimu mbili mwaka 2020 hadi skimu 15 mwaka 2025 zilizojengwa katika
8
Halmashauri za wilaya za Shinyanga, Shinyanga Mjini, Manispaa ya Kahama, Msalala na Kishapu;
(b) Kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa mbolea ya ruzuku kutoka tani 9,870,000 mwaka 2020 hadi tani 23,223,000 mwaka 2025;
(c) Kuongeza matumizi ya mbolea kwa ajili ya shughuli za kilimo kutoka tani 5443 mwaka 2020 hadi tani 9,909 mwaka 2025;
(d) Kuongezeka kwa mavuno ya mazao kutoka tani 684,200 mwaka 2020 hadi tani 884,116 mwaka 2025;
(e) Kuimarisha huduma za ugani kwa kununua vitendea kazi ikiwemo pikipiki 214, vipima udongo 5 na vishikwambi 193 kwa ajili ya maafisa ugani;
(f) Kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani 797,000 mwaka 2020 hadi tani 1,313,073 mwaka 2025 na mazao ya biashara kutoka tani 99,250 mwaka 2020 hadi tani 170,673 mwaka 2024;
2.2.2 Mifugo
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:
(a) Kuongezeka kwa uzalishaji wa maziwa kutoka lita 10,031,225 mwaka 2020 hadi lita 18,335,300 mwaka 2025;
(b) Kuongezeka kwa uzalishaji wa nyama kutoka tani 3,150 mwaka 2020 hadi tani 5,600 Mwaka 2025;
(c) Kuongeza uzalishaji wa zao la ngozi kutoka vipande 58,035 Mwaka 2020 hadi vipande 108,770 mwaka 2025;
(d) Kuanzisha mashamba darasa ya malisho ya mifugo 4.
9
(e) Kuongezeka kwa usambazaji wa dawa za ruzuku za kuogeshea mifugo lita 2,060.5 na dozi 823,000 za chanjo ya kudhibiti ugonjwa wa sotoka ya mbuzi na kondoo;
(f) Kukamilika kwa ujenzi wa majosho 16 ya kuogeshea mifugo katika Halmashauri za Kishapu, Shinyanga DC, Shinyanga MC na Ushetu;
(g) Kuimarisha huduma za ugani kwa kugawa pikipiki 54 kwa ajili ya maafisa mifugo;
(h) Kuanzisha mashamba darasa ya malisho ya mifugo 4
(i) Kutoa elimu ya ufugaji bora na uboreshaji wa mbari za mifugo kwa kusambaza mbegu bora za mifugo Bosmara, Aryshire na Frisian kwa njia ya uhimilishaji;
2.2.3 Madini
Mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa sekta hii ni pamoja na:
(a) Kuongezeka kwa uzalishaji wa madini kutoka tani 7.9 mwaka 2020 hadi tani 42.5 mwaka 2025;
(b) Kuongezeka kwa fedha za kigeni zilizotokana na uuzaji wa madini kutoka Dola za Marekani milioni 44.33 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani milioni 191.15 mwaka 2025;
(c) Kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri yatokanayo na uchimbaji wa madini kutoka Shilingi milioni 745.4 mwaka 2020 hadi Shilingi 3,334,265,389.56 mwaka 2025;
(d) Kuongezeka kwa masoko na vituo vya ununuzi madini kutoka 06 mwaka 2020 hadi vituo 12 mwaka 2025; na
(e) Kuongezeka kwa utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo kutoka leseni 332 mwaka 2020 hadi 1,766 mwaka 2025.
10
(f) Kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli kutoka shilingi bilioni 103.4 mwaka 2020/21 hadi kufikia shilingi bilioni 607.04 mwaka 2024/25.
(g) Kuanzisha masoko ya madini katika maeneo ya Wilaya za Kahama na Shinyanga;
2.2.4 Viwanda na Biashara
Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:
(a) Kuanzishwa kwa Kongani Maalumu ya Uwekezaji ya Buzwagi (SEZ) ambapo mpaka sasa kampuni moja ya East Africa Conveyers Service imeanza uzalishaji na Kampuni nne zimeanza taratibu za kupata Leseni na zimefanya usajili wa Mradi NEMC. Aidha Kampuni 15 zimeonesha nia ya kuwekeza katika Kongani Maalumu ya Uwekezaji ya Buzwagi.
(b) Kuanzishwa kwa viwanda vikubwa 4 kutoka 36 mwaka 2020 hadi 40 mwaka 2025; viwanda vya kati 12 kutoka 180 hadi 192 mwaka 2025 na viwanda vidogo 222 kutoka 999 mwaka 2020 hadi viwanda 1,225 mwaka 2025;
(c) Kuanzisha na kuendeleza kongani Nyashibi, Buzwagi na Busoka za viwanda na Soko la kimataifa la mazao.
(d) Kuongezeka kwa ajira za viwandani, ambapo jumla ya wananchi 50,000 wameajiriwa, kati yao elfu 35,000 ni ajira za muda na 15,000 elfu ni ajira za kudumu.
11
2.2.5 Miundombinu
Mkoa umepokea kiasi cha shilingi bilioni 221.19 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara, madaraja na makalvati ili kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:
(a) Kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami kutoka kilomita 224 mwaka 2020 hadi kilomita 281 mwaka 2025;
(b) Kuongezeka kwa mtandao wa barabara za changarawe kutoka kilomita 957.11 mwaka 2020 hadi 1,411.50 mwaka 2025;
(c) Kukamilisha ujenzi wa madaraja kutoka 45 mwaka 2020 hadi 57 mwaka 2025;
(d) Kukamilisha ujenzi wa makalavati 2,356 mwaka 2020 hadi 4,469 mwaka 2025;
(e) Kusimika taa za barabarani 611;
Nishati
Mkoa umepokea kiasi cha Shilingi bilioni 492 kupitia Shirika la Umeme Tanesco, Mafanikio yaliyopatikan ni pamoja na:
(a) Kukamilisha uunganishaji wa umeme katika vijiji vyote 506 pamoja na vitongoji 982 kati ya vitongoji 2,704 sawa na asilimia 36;
(b) Kuendelea na utekelezaji wa mkakati wa nishati safi ya kupikia ambao umelenga kuboresha afya ya jamii na kulinda mazingira safi ya kupikia kwa kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kugawa mitungi 6,500 ya gesi; na
(c) Kukamilisha utekelezaji wa miradi 133 ya usambazaji umeme
12
Ardhi
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:
(a) Kuwezesha upimaji wa viwanja 10,658 sawa na asilimia 157 ya lengo la kupima viwanja 6,776;
(b) Kuongezeka kwa utoaji hati miliki za ardhi kutoka 10,568 mwaka 2020 hadi 20,068 mwaka 2025;
(c) Kuongezeka kwa utoaji hati miliki za kimila kutoka 816 mwaka 2020 hadi 4,930 mwaka 2025;
(d) Kuongezeka kwa vijiji vyenye mpango wa matumizi bora ya ardhi kutoka vijiji 18 mwaka 2020 hadi vijiji 116 mwaka 2025;
(e) Upatikanaji wa maeneo ya uwekezaji kama vile eneo la Chapulwa, Zongomela, Nyashimbi Halmashauri ya Manispaa Kahama na Negezi na Ibadakuli katika Halmashauri ya Manispaa Shinyanga.
(f) Upatikanaji wa maeneo ya huduma za jamii kama vile shule, barabara, maeneo ya wazi, michezo.
(g) Ajira za muda kwa wataalam pamoja na vijana vibarua 2,462.
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:
(a) Kuongezeka kwa utoaji wa mikopo kufikia shilingi bilioni 8.56 kwa vikundi 1,124 vya wanawake, vijana na Watu Wenye Ulemavu; na
(b) Kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo jumla ya Shilingi bilioni 59.57 ziliwasilishwa kwa kaya za walengwa 35,055, kutekeleza miradi 77 ya miundombinu ya
13
elimu, afya na barabara pamoja na kuwezesha walengwa 15,103 kujiongezea kipato kupitia ufugaji na kilimo.
(c) Mikopo kupitia Vitambulisho vya Wajasiriamali ambapo Mkoa umefanikiwa kusajili vitambulisho vya wajasiriamali 225. Zoezi hili linaenda sambamba na zoezi la utoaji wa Mikopo kwa wajasiriamali inayotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kupitia benki ya NMB. Mkopo huo utatolewa kwa mjasiriamali mmoja mmoja na utakuwa na riba ya asilimia 7 tu. Hivyo mjasiriamali atakayekuwa amepata kitambulisho hiki ndiye atakuwa amepata sifa ya kupata mkopo huo.
(d) Kwa mara ya kwanza Mkoa ulishiriki Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam ya mwaka 2025. Katika maonesho hayo Mkoa uliweza kutangaza biashara na fursa zilizopo katika Mkoa wa Shinyanga.
Utawala bora
Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na:
(a) Kukamilika kwa ujenzi wa Jengo la mwendesha mashtaka kwa gharama ya shilingi bilioni 2.15;
(b) Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba za wakuu wa wilaya za Shinyanga na Ushetu kwa gharama ya shilingi milioni 720; nyumba ya Katibu Tawala Kahama kwa gharama ya shilingi milioni 150; na nyumba 2 za Maafisa Tarafa kwa gharama ya shilingi milioni 180;
14
(c) Kuendelea na ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Halmashauri za Shinyanga MC, Shinyanga DC, Ushetu na msalala kwa gharama ya shilingi bilioni 12 na ofisi za wakuu wa wilaya za Kishapu kwa gharama ya shilingi bilioni 1.66;
Miradi ya Kimkakati inayotekelezwa;
(a) Serikali inaendelea na ujenzi wa Mradi wa umeme Jua uliopo kijiji cha Ngunga, Wilayani Kishapu wenye megawati 150 unaogharimu shilingi bilioni 323.
(b) Ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Ibadakuli – Shinyanga wenye urefu wa Kilomita 2.2 pamoja na ujenzi wa jengo la abiria unaogharimu Shilingi bilioni 52.87.
(c) Ujenzi wa wa barabara kwa Kiwango cha Lami Kahama - Bulyanhulu JCT- Kakola km 73 unaogharimu bilioni 100.6.
(d) Ujenzi wa shule ya Amali ya Nyamilangano yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6.
(e) Mradi wa usambazaji Maji wa Ziwa Victoria kutoka Manispaa ya Kahama kwenda Ushetu kwa gharama ya shilingi bilioni 37.51.
(f) Mradi wa TACTIC ikiwemo kujenga barabara za katikati ya mji (CBD) (km 12.03); Ujenzi wa barabara eneo la viwanda Zongomela (km 3.06); Ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua (km 4.9); Uboreshaji wa miundombinu ya barabara eneo la viwanda Zongomela; Ujenzi wa Kituo cha Mabasi Mbulu; Uboreshaji wa soko la Sango; Ujenzi wa stendi ndogo na soko eneo la viwanda Zongomela kwa Manispaa ya Kahama. Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 48.3.
15
(g) Mradi wa TACTIC ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha eneo la Kizumbi, Ujenzi kwa Kiwango cha lami ngumu Barabara za nguzo nane -Mwawaza (4.68km), Swernatone - Ndala (1.67km) na Ujenzi wa Soko la matunda Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga wenye thamani ya shilingi bilioni 24.3.
3.0 HITIMISHO
Mkoa wa Shinyanga na wananchi kwa ujumla, tunaishukuru sana Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupenda na kutuletea maendeleo haya makubwa.
Ni dhahiri kabisa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2020 – 2025) imetekelezwa kwa uwazi, umahiri na mafanikio makubwa na wananchi tunashuhudia mafanikio haya.
Comments