Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Julai 16, 2025, kuhusu mafanikio ya mkoa huo katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Waandishi wa Habari wakiwa katika mkoa huo.
Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Kelvin Kanje akiruhusu wanahabari kuuliza maswali.
1.0 MAFANIKIO KWA KILA SEKTA
Jumla ya Shilingi Trilioni 5.6 zimepokelewa Mkoani kipindi cha mwezi
Novemba, 2020 hadi Aprili, 2025 kwa ajili ya maendeleo ya sekta mbalimbali kama
ifuatavyo: -
1.1
Sekta
ya Afya
Jumla ya Shilingi Bilioni 63.2 zimetolewa
(ii) Miradi ya ujenzi wa vyoo mashuleni na maeneo ya
wazi yenye thamani ya Shilingi 7,492,265,910.54 imekamilika katika shule na
vituo vya afya mbalimbali.
(iii) Mradi wa uondoshaji maji taka katika maeneo ya
milimani umetekelezwa kwa Shilingi 3,720,864,077.92 katika maeneo ya Pasiansi,
Kilimahewa A, Kilimahewa B na Mabatini B. Ujenzi wa Mfumo wa Kutibu Majitaka
katika Gereza Kuu la Butimba umegharimu Shilingi 1,969,862,600.
(iv)
Mradi wa upanuzi wa mabwawa ya majitaka kwa thamani ya Shilingi 6,739,048,681.80.
(v)
Visima vitano vya chanzo mbadala vimejengwa kwa Shilingi 294,844,126.00 na
(vi)
Wilaya ya Misungwi, MWAUWASA inaendelea kutekeleza mradi wa maji katika
Kata ya Misungwi, Igokelo Iteja, Mwamanga, Mitindo B, Old Misungwi, Mbela B, C,
D na Ng’ombe, na kunufaisha wakazi 22,482.
(vii) Wilaya ya Ukerewe imepokea Shilingi 42,738,000.00
kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya bomba katika maeneo ya Kakerege, Bugoye,
Hamkoko Bulamba/Munfunzi na Namalebe ambapo wanufaika ni wananchi 3,500 na kaya
250.
c) Hali ya Upatikanaji wa Maji Safi Vijijini Mwaka 2020 hadi 2025
(i)
Wilaya ya Kwimba imetekeleza miradi 29 ya maji katika vijiji mbalimbali
pamoja na uchimbaji wa visima 22, Kwa gharama Shilingi. 22,046,262,574.43
(ii)
Wilaya ya Magu ilipokea Shilingi. 13,479,505,945.97 kwa utekelezaji wa
miradi ya maji, uchimbaji wa visima 19 katika vijiji 5.
(iii) Wilaya ya Misungwi ilipokea jumla ya Shilingi.
21,210,784,588, ambapo miradi ya thamani ya Shilingi. 7,122,836,106.08
imekamilika na ile ya Shilingi. 14,087,948,482.50 inaendelea kutekelezwa.
(iv) Wilaya ya Sengerema imetekeleza miradi 27 ya
maji yenye thamani ya Shilingi. 40,464,136,499.74 pamoja na uchimbaji wa visima
13.
(v) Ukerewe imetekeleza miradi 12 ya maji yenye
thamani ya Shilingi. 15,277,263,613.41 katika maeneo ya Kazilankanda,
Murutanga, Hamyebo na Busunda.
2.4
.Miundombinu
ya Barabara
Jumla ya Shilingi Bilioni 156.3 zimetolewa
(i)
Jumla ya madaraja 13
yamekarabatiwa na kujengwa kwa gharama ya Shilingi Billioni 36.9 kwa mchanganuo
ufuatao:
a)
Daraja la Simiyu
linajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.8
a)
Mkoa una jumla
ya hospitali za umma 10, Vituo vya afya 55 na zahanati 298. Hospitali za Wilaya
zimeendelea kupatiwa fedha
ili kuendelea na ujenzi mpaka sasa umegharimu jumla ya Shilingi 12,791,950,164.08
b)
Ukarabati wa hospitali za Wilaya ya Nyamagana, Magu
na ukerewe kwa gharama ya Shilingi 5,171,802,836.30
c)
Ujenzi wa Wodi
ya Saratani, Jengo la Macho, uwekaji wa mitambo ya kufua Oksijeni na ukarabati
wa ICU katika Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Bugando kwa gharama ya Shilingi 9,872,000,000.
d) Ujenzi
wa Hospitali ya Ukerewe ambayo itakuwa yenye hadhi ya Rufaa ya Mkoa Shilingi
25,034,660,304.69 zimeletwa awamu ya kwanza inaendelea kujengwa katika kijiji
cha Bulamba Wilaya ya Ukerewe.
e)
Idadi ya Wataalamu wa afya imeongezeka kutoka 2,855 mwaka 2020 hadi 4,150
mwaka 2025 sawa na ongezeko la wataalamu 1,295. Ajira mpya 1,015 na watumishi 280 wamehamia
f) Idadi ya nyumba za watumishi zimeongezeka kutoka 355 mwaka 2020
hadi 436 mwaka 2025 sawa na ongezeko la nyumba 81
g)
Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba imeongezeka
kutoka Shilingi 4,288,886,698.4 mwaka 2020/2021 hadi Shilingi 10,352,912,100.55
mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la Shilingi 6,064,025,332.15
b)
Idadi ya wananchi waliojiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa (Ichf)
imeongezeka kutoka wananchi 294,304 mwaka 2020 hadi hadi 602,829 mwaka 2025
sawa na ongezeko la wananchi 308,647.
c)
Kiwango cha maambukizi ya malaria kimepungua kutoka asilimia 8 mwaka 2020
hadi asilimia 1 mwaka 2025.
d) Huduma za upasuaji wa dharura vijijini zimeboreshwa kutoka vituo
17 mwaka 2020 hadi vituo 40 mwaka 2025 sawa na ongezeko la vituo 23
e) Upatikanaji wa huduma za ubingwa na ubingwa Bobezi kwa
kuleta kambi za madaktari bingwa katika
Mkoa kutoa huduma za kibingwa ambazo awali zilikuwa zikipatikana katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili pekee,
f)
Uwekaji wa mitambo ya kufua Oksijeni katika Sekou Toure umefanyika.
g)
Jumla ya maabara 3 zimepata
ithibati (accreditation) zimefikia utambulisho wa ubora wa utoaji huduma za
kimaabara ngazi ya Kimataifa ambazo ni maabara iliyopo Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Bugando, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure, Hospitali ya Nyamagana
na Sengerema DDH.
h) Huduma ya uchunguzi kwa kipimo cha Utrasound imeboreshwa kutoka
vituo 2 mwaka 2020 hadi vituo 45 mwaka 2025.
a)
Upatikanaji dawa na vifaa tiba katika sehemu za kutolea huduma za afya
umeongezeka kutoka asilimia 77.89 mwaka 2020 hadi asilimia 92.29 mwaka 2025
sawa na ongezeko la asilimia 14.73
b)
Idadi ya wananchi waliojiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa (Ichf)
imeongezeka kutoka wananchi 294,304 mwaka 2020 hadi hadi 602,829 mwaka 2025
sawa na ongezeko la wananchi 308,647.
c)
Kiwango cha maambukizi ya malaria kimepungua kutoka asilimia 8 mwaka 2020
hadi asilimia 1 mwaka 2025.
d) Huduma za upasuaji wa dharura vijijini zimeboreshwa kutoka vituo
17 mwaka 2020 hadi vituo 40 mwaka 2025 sawa na ongezeko la vituo 23
e) Upatikanaji wa huduma za ubingwa na ubingwa Bobezi kwa
kuleta kambi za madaktari bingwa katika
Mkoa kutoa huduma za kibingwa ambazo awali zilikuwa zikipatikana katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili pekee,
f)
Uwekaji wa mitambo ya kufua Oksijeni katika Sekou Toure umefanyika.
g)
Jumla ya maabara 3 zimepata
ithibati (accreditation) zimefikia utambulisho wa ubora wa utoaji huduma za
kimaabara ngazi ya Kimataifa ambazo ni maabara iliyopo Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Bugando, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure, Hospitali ya Nyamagana
na Sengerema DDH.
h) Huduma ya uchunguzi kwa kipimo cha Utrasound imeboreshwa kutoka
vituo 2 mwaka 2020 hadi vituo 45 mwaka 2025.
a)
Digital X- ray
zimeongezeka kutoka 2 mwaka 2020 hadi 26
mwaka 2025. (Nyamagana
5, Ilemela 4 Kwimba 3, Misungwi 4, Sengerema 3, Magu 3, Ukerewe 4)
b)
Jumla ya CT Scan 3 zimenunuliwa zimeanza kutoa huduma katika Hospitali ya
Rufaa ya Kanda – Bugando, Hospitali ya Mkoa Seko Toure na Hospitali ya Jeshi.
c)
Mashine ya MRI imenunuliwa na Serikali na imesimikwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Kanda Bugando.
2.2 Sekta ya Elimu
Jumla ya
Shilingi Bilioni 196.8 zimetolewa
Miundombinu imeboreshwa
ambayo imesaidia kumepunguza kwa
kiasi kikubwa umbali wa kutembea kwenda shule, msongamano wa wanafunzi
madarasani, kuwezesha mazingira bora zaidi kwa walimu na wanafunzi. Maboresho
yafuatayo yamefanyika :-
(i)
Mpango wa Elimu Bila Malipo kwa shule za msingi katika Mkoa umegharimu
jumla ya Shilingi 32,812,096,940.45 kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi
2024/2025. Utekelezaji wa mpango huu umewezesha uboreshaji wa mazingira ya
kujifunzia na kufundishia, sambamba na kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora,
jumuishi na isiyo na vikwazo vya ada kwa wanafunzi
(ii) Mpango wa Elimu Bila Malipo kwa shule za
sekondari umegharimu jumla ya Shilingi 44,695,682,656.24 kuanzia mwaka wa fedha
2021/2022 hadi 2024/2025.
(iii)
Idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka shule 873 mwaka 2020 hadi shule
930 mwaka 2025, sawa na ongezeko la shule 57.
(iv) Idadi ya shule za sekondari imeongezeka
kutoka shule 219 mwaka 2020 hadi shule 308 mwaka 2025, sawa na ongezeko la
shule 89.
(i)
Idadi ya vyumba vya madarasa katika shule za msingi imeongezeka kutoka
vyumba 7,464 mwaka 2020 hadi kufikia vyumba 8,866 mwaka 2025, sawa na ongezeko
la vyumba 1,402.
(ii)
Idadi ya vyumba vya madarasa katika shule za sekondari imeongezeka kutoka
vyumba 3,175 mwaka 2020 hadi 5,742 mwaka 2025, sawa na ongezeko la vyumba
2,567.
(iii)
Idadi ya vyumba vya maabara katika shule za sekondari imeongezeka kutoka
vyumba 421 mwaka 2020 hadi vyumba 579 mwaka 2025, sawa na ongezeko la vyumba
158.
(iv)
Idadi ya matundu ya vyoo katika shule za msingi imeongezeka kutoka 10,202
mwaka 2020 hadi 13,423 mwaka 2025, sawa na ongezeko la matundu 3,221.
(v)
Idadi ya matundu ya vyoo katika shule za sekondari imeongezeka kutoka 3,903
mwaka 2020 hadi 5,901 mwaka 2025, sawa na ongezeko la matundu 1,998.
(vi)
Jumla ya vifaa 243 vya TEHAMA vimewekwa katika shule za sekondari kwa
gharama ya jumla ya Shilingi 241,250,000.00 kwa lengo la kuboresha mazingira ya
ufundishaji na ujifunzaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Utekelezaji huu
umewezesha wanafunzi kupata fursa ya kutumia vifaa vya kidijitali katika kukuza
maarifa, kuongeza ufanisi wa ujifunzaji wa masomo ya sayansi, hisabati, na
stadi za maisha, sambamba na kuimarisha ujuzi wa TEHAMA miongoni mwa walimu na
wanafunzi.
(vii)Idadi ya mabweni imeongezeka kutoka mabweni
61 mwaka 2020 hadi mabweni 184 mwaka 2025, sawa na ongezeko la mabweni 123.
(viii) Idadi ya mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji
maalumu katika shule za msingi imeongezeka kutoka mabweni 0 mwaka 2020 hadi mabweni
4 mwaka 2025, sawa na ongezeko la mabweni 4.
(ii)
Ujenzi wa Chuo cha Uhasibu cha TIA – Kampasi ya Mwanza umekamilika kwa
gharama ya Shilingi 9,800,000,000
(iii)
Ujenzi wa vyuo vitatu vya ufundi (VETA) katika Halmashauri za Magu,
Misungwi na Buchosa unaendelea kwa gharama ya Shilingi 10,200,000,000 kwa lengo
la kuimarisha elimu ya ufundi stadi kwa vijana na kuwawezesha kushiriki
kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. Ujenzi unaendelea.
(iv)
Ujenzi wa chuo cha ufundi kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum katika
Halmashauri ya Magu unaendelea na umefikia hatua za ukamilishaji.
(v)
Ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Michezo Malya kilichopo
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa gharama ya Shilingi 34,082,032,000 unaendelea.
(vi)
Ujenzi wa Maktaba ya Mkoa kwa
gharama ya Shilingi 2,887,000,000 unaendelea
(vii) Ujenzi wa Chuo cha Dar es salaam Institute
of Techology (DIT) – Kampasi ya Mwanza kwa gharam ya Shilingi 26,843,347,993 unaendelea.
(viii) Ujenzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) – Kampasi ya Mwanza kwa gharama ya Shilingi 5,365,840,722
unaendelea.
(i)
wanafunzi 63,392 mwaka 2020 hadi wanafunzi 324,346 mwaka 2025, ikiwa ni
ongezeko la wanafunzi 260,954, Kidato cha Tano umeongezeka kutoka wanafunzi
11,719 mwaka 2020 hadi kufikia wanafunzi 82,969 mwaka 2024, sawa na ongezeko la
wanafunzi 71,250.
(ii)
Ufaulu wa
mitihani Kidato cha Pili umeongezeka kutoka asilimia 91.5 mwaka 2020 hadi
asilimia 97.1 mwaka 2025 kwa mkoa mzima wa Mwanza, sawa na ongezeko la wastani
la asilimia 5.6. Kidato cha Nne umeongezeka
kutoka asilimia 88.37 mwaka 2021 hadi asilimia 96.34 mwaka 2024, sawa na
ongezeko la wastani wa asilimia 7.97. Kidato cha Sita katika Mkoa umeongezeka kutoka asilimia 97.62 mwaka
2021 hadi asilimia 99.76 mwaka 2024, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia
2.14.
(iv)
Idadi ya
walimu wa shule za sekondari imeongezeka kutoka walimu 5,675 mwaka 2020 hadi
kufikia walimu 6,715 mwaka 2025, sawa na ongezeko la walimu 1,040.
(v)
Jumla ya wanafunzi
wa kike 485 walioacha shule wamepata nafasi ya kurudi shule.
2.3 Sekta ya
Huduma ya Maji Mijini na Vijijini
Jumla ya Shilingi Bilioni
264.8 zimetolewa
a) Hali
ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama imeongezeka:
§
Mijini, kutoka 57% hadi 85%
§
Vijijini, kutoka 57% hadi 77.8%
b) Hali
ya upatikanaji maji mijini (MWAUWASA)
Kuanzia Julai 2020 hadi Mei 2025, jumla ya
miradi 19 yenye thamani ya Shilingi 164,419,664,492.55 imekamilika
kwa kutekeleza yafuayao:-
b)
Daraja la
Mabatini: linajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6
c)
Daraja la
Mkuyuni: linajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5.2
d)
Daraja la
Nyaluha na Kishinda: Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 3.3
e)
Daraja la Sakanti
na Malemve: mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5.5
f)
Jumla ya
madaraja 7 madogo yamejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1.6 katika
Halmashauri za Wilaya ya Ilemela, Magu, Kwimba na Buchosa
g)
Jumla ya
Makalavati 143 yamejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1 katika Mkoa wa
Mwanza
h)
Jumla ya madrift
2 yamejengwa kwa gharama za Shilingi Millioni 100 katika Halmashauri ya Buchosa
i)
Jumla ya taa 1,374 zimewekwa katika Mkoa wa
Mwanza.
ii) Wakala wa Barabara za Vijijini na
Mijini (TARURA)
Baadhi
ya miradi mikubwa ya barabara iliyotekelezwa na TARURA ya
gharama ya Shilingi Bilioni 72.7–
kazi zinaendelea vizuri.
a)
Mtandao wa barabara za lami umeongezeka kutoka Km 76.82 mwaka 2020 hadi Km 103.08 mwaka 2025 sawa
na Ongezeko la Km 26.26.
b)
Mtandao wa barabara
za mawe umeongezeka kutoka Km 14.75 mwaka 2020 hadi Km
21.14 mwaka 2025 sawa na ongezeko la Km
6.29.
c)
Mtandao wa barabara za changarawe umeongezeka kutoka Km 2375.352 mwaka
2020 hadi Km 3996.442 mwaka 2025 sawa na ongezeko la Km 1621.
b) Ujenzi wa barabara ya Buswelu – Nyamadoke
- Nyamhongolo kiwango cha lami Km 9.5 ujenzi unaendelea.
c) Ujenzi wa barabara ya Buswelu – Busenga – Coca cola kwango cha lami Km 3.3 ujenzi unaendelea
d) Ujenzi wa barabara ya Majengo kiwango cha lami yenye urefu wa Km
0.5 ujenzi unaendelea.
e) Matengenezo ya barabara ya Kanyerere –
Gabajiga - Budutwa kwa kiwango cha lami Km
9.9 kazi inaendelea
2.4
Uboreshaji
Bandari (Mwanza Kaskazini)
Jumla ya Shilingi Bilioni 18.6 zimetolewa
Uboreshaji
unahusisha majengo ya abiria ili kuhudumia abiria wengi zaidi, kuongeza eneo la
maegesho ya magari, kuongeza urefu wa gati na kina cha maji. Ujenzi wa uzio,
taa na kamera za usalama ujenzi za mto mirongo katika eneo la bandari Utekelezaji,
bandari na 58%.
2.5
Ujenzi wa Vivuko
Jumla ya Shilingi 18,674,414,228.51
zimetolewa
Mradi wa ujenzi wa vivuko vipya
vitano (5) vya Kisorya – Rugenzi Wilaya ya Ukerewe - chenye thamani ya Shilingi 892,760,706.00
Ijinga – Kahangala 5,255,080,099.51 – Magu,
Bwiro – Bukondo Shilingi 676,164,840.00 - Ukerewe Nyakarilo – Kome Shilingi 8,033,344,250.00 -
Buchosa, Buyagu - Mbalika Shilingi
3,817,064,333.00 unaendelea.- Misungwi. Vivuko 12
vilivyopo vimeendelea kufanyiwa ukarabati
ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
2.6
Usafiri wa anga umeboreshwa
Jumla ya Shilingi. 34,515,699,054.21 zimetolewa
b)
Jumla
ya Shilingi 5,195,477,306.88 zimetolewa
kwa ajili ya kuboresha uwanja wa ndege kwa maandalizi ya kuwa uwanja wa kimataifa
shughuli zifuatazo zimetekelezwa:- Ujenzi wa Uzio wa ndani wa Usalama (Inner
Security Fence) wa km 12, mageti 13, ujenzi wa makalavati ya urefu wa mita 15
kuzunguka uwanja, Ujenzi wa Mfumo wa tozo za maegesho ya magari (electronic car
parking management System), kuweka mfumo wa kisasa wa kuhudumia mizigo, utengenezaji
wa “Runway Designation Markings”,Ujenzi wa Uzio wa Usalama (Security Fence)
katika Ofisi za Utawala na ukarabati wa Jengo la Zimamoto
2.4
Usafiri wa majini
Jumla ya Shilingi biilioni 156.9
zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na ukarabati
a)
Mradi wa ujenzi wa meli mpya ya “MV Mwanza Hapa kazi Tu” kwa gharama ya Shilingi 120,6. Meli hii
itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari madogo 20
na malori 3. Mradi huu utekelezaji wake umefikia asilimia 96
b)
Mradi wa ukarabati wa meli ya
uokozi (Tug boat) ya MT Ukerewe na MV
Umoja Kazi iendelee kwa gharama ya Shilingi
26.9. Ukarabati umekamilika
c)
Ununuzi wa Boti za Utafutaji
na Uokozi pamoja na boti ya matibabu Kwa
gharama ya Shilingi Billioni 4.5 ujenzi umekamilika
2.4
Nishati ya Umeme
Jumla ya Shilingi 110,104,728,354.78 zimetolewa
Umeme katika Vijiji na
Vitongoji: -
(i)
Vijiji 522 vya nchi kavu
vimeunganishwa umeme kwa asilimia 100, Vijiji 23 ambavyo ni visiwa viko kwenye mpango wa mradi wa nishati ya
jua kwa kaya binafsi.
(ii)
Vitongoji 1,808 kati ya 3,448
vimeungwa umeme sawa na 52%.
(iii) REA imetumia Shilingi 94,280,441,937.14
katika miradi mbalimbali ya usambazaji umeme vijijini.
(iv) Miradi ya PERI-URBAN kwa Shilingi 9,943,685,936.05
(v)
Mradi wa kupeleka umeme kwenye vyanzo vya maji kwa gharama ya Shilingi 4,111,334,164
(vi) Mradi wa kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo
kwa gharama ya Shilingi 1,769,266,317.59
(vii) Jumla
ya taasisi za umma 32 zimehamasishwa kutumia nishati mbadala ya kupikia ya gasi
(viii)
Jumla ya majiko ya gasi 25,235 yameuzwa
kwa wananchi kwa bei ya ruzuku
2.5
Sekta
ya Kilimo
a)
Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 640,205.3 (37.59%)
2020/21 hadi kufikia tani 1,025,784.08 (60.23%) mwaka 2024/25 sawa na ongezeko
la Tani 385,578 (22.64%)
b)
Ujenzi na ukarabati wa miradi ya umwagiliaji 2 ya Sengerema Katunguru na Mahiga
kwimba kwa gharama ya Shilingi. 54,473,623,973.41 unaendelea Upatikanaji wa
viuatilifu umeongezeka kutoka chupa 324,821 Mwaka 2020 hadi chupa 832499 Mwaka
2025.
b) Katika kuboresha maslahi ya wakulima, mfumo
wa kununua mazao kupitia vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) vimeongezeka
kutoka vyama 164 mwaka 2018 hadi vyama 257 mwaka 2025.
2.4
Sekta ya Mifugo
a)
Uzalishaji wa mitamba umeongezeka kutoka mitamba 58,625 mwaka 2020 hadi
215,775 mwaka 2025 sawa na ongezeko la mitamba 157,149.
b)
Mauzo ya mitamba kwa wananchi yameongezeka kutoka mitamba 44,320 mwaka
2020 hadi mitamba 143,926 mwaka 2025 sawa na ongezeko la mauzo ya mitamba
99,606.
c)
Idadi ya majosho mapya yaliyojengwa mwaka 2020 yalikuwa 55 yameongezeka
hadi kufikia majosho mapya 76 mwaka 2025
sawa na ongezeko la majosho 21.
d)
Idadi ya viwanda vya nyama na mazao mengine ya mifugo vilivyoanzishwa
imeongezeka kutoka viwanda 3 mwaka 2020 hadi 6 mwaka 2025 sawa na ongezeko la
viwanda 3.
e)
Idadi ya mabwawa ya kunyweshea mifugo yamejengwa kutoka mabwawa 121
mwaka 2020 hadi mabwawa 238 mwaka 2025 sawa na ongezeko la mabwawa 117.
a)
Ufugaji wa samaki kwa kutumia njia ya kisasa umeongezeka kutoka vizimba
(fish cauges) 1,664 mwaka 2020 hadi 2,715 mwaka 2025 sawa na ongezeko la
vizimba 1,051.
b)
Jumla ya tani 43,657.6 za minofu ya Samaki zimechakatwa na tani 81,812
zimesafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa
kipindi cha mwaka 2024
c)
Kilo za mabondo zilizosafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia
Uwanja wa Ndege wa Mwanza zimeongezeka kutoka kilo 431,721 mwaka 2020 hadi kilo
495,448 mwaka 2024 sawa na ongezeko la kilo 63,727.
d)
Idadi ya mabwawa ya ufugaji wa Samaki imeongezeka kutoka 286 mwaka 2020
hadi mabwawa 531 mwaka 2025 sawa na ongezeko la mabwawa 245.
e)
Kiasi cha mapato yaliyotokana na shughuli za uvuvi kimeongezeka kutoka Shilingi
4,416,172,821.59 mwaka 2020 hadi Shilingi 8,233,724,351.33 mwaka 2025 sawa na
ongezeko la Shilingi 3,817,551,529.74.
2.5
Mazingira, Maliasili na Utalii
a)
Idadi ya watalii waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saanane imeongezeka
kutoka 13,175 mwaka 2020 hadi 24,748 mwaka 2025 sawa na ongezeko la watalii 11,573.
b)
Mapato ya Hifadhi ya Taifa ya Saanane yatokanayo na Utalii yameongezeka
kutoka Shilingi 210,818,714.53 mwaka 2020 hadi Shilingi 274,488,877.09 mwaka
2025 sawa na ongezeko la Shilingi 63,670,162.56
2.6
Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, Biashara na Uwekezaji
a)
Jumla ya Shilingi Bilioni 85.8
zimewezesha Wananchi Kiuchumi
§ Vikundi
vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyopewa mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba vimeongezeka
kutoka 630 hadi 1,856. Aidha, kiwango cha mikopo iliyotolewa nacho kimeongezeka
kutoka Shilingi Bilioni 3.3 hadi Shilingi. Bilioni 14.1.
§ Kupitia
Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), Jumla ya kaya 59,932 zimenufaika Shilingi Bilioni 44 zimetolewa kwa
walengwa.
§ Mifuko mingine iliyowezesha wananchi ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa
Kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (National Entrepreneurship Development Fund) umetoa mikopo ya Shilingi. 371,000,000
kwa wanaufaika 160, Mfuko wa Mzunguko wa Mikoani
(SIDO RRF); umetoa mikopo kwa vijana 38 yenye thamani ya Shilingi 26,000,000. Mfuko wa Kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF
Microfinance Fund); jumla Shilingi. 27,369,130,990 zimetolewa kwa wanaufaika
173,6000.
a)
Biashara
na Uwekezaji
§ Katika Mkoa wa Mwanza Idadi ya Viwanda
Vikubwa imeongezeka kutoka 46 mwaka
2020 hadi viwanda 50 mwaka 2025 sawa na ongezeko la viwanda 4.
§ Idadi ya viwanda vya kati imeongezeka
kutoka 109 mwaka 2020 hadi viwanda 116 mwaka 2025 sawa na ongezeko la viwanda
7.
§ Idadi ya viwanda vidogo na vidogo sana
imeongezeka kutoka viwanda 1,776 mwaka
2020 hadi viwanda 2,322 kwa Mwaka 2025
sawa na ongezeko la viwanda 546.
§ Idadi ya biashara zenye leseni imeongezeka
kutoka 23,704 mwaka 2020 hadi 29,606 mwaka 2025 sawa na ongezeko la biashara
zenye leseni 5,902.
2.4
Ukusanyaji
Mapato ya Ndani katika Halmashauri
Makusanyo yameongezeka kutoka jumla ya Shilingi Bilioni 44.2 mwaka 2020/21 hadi Shilingi Bilioni 70.7 mwaka 2024/25 kufikia mwezi Mei, 2025 sawa na ongezeko la 60%. Aidha, kwa kipindi cha miaka mitano (5) zimekusanywa jumla ya Shilingi Bilioni 216.2
2.4
Utekelezaji
wa Miradi ya Kimkakati Kuchachua Uchumi wa Mkoa
Mkoa umeendelea
kutekeleza Miradi mbalimbali ya Kimkakati kwa gharama ya Shilingi 3,969,880,676,469.24
Kwa
mchanganuo ufuatao:-
a)
Ujenzi wa Reli SGR Mwanza - Isaka kwa Shilingi 3,062,031,806,702.83,
unaendelea
b)
Ujenzi wa Daraja la JPM Kigongo - Busisi kwa Shilingi
716,333,000,000.0 umekamilika.
c)
Ujenzi wa Meli Mpya ya MV MWANZA kwa gharama
ya Shilingi 120,562,787,135.31, unaendelea
d)
Ujenzi wa kituo cha Mabasi Nyegezi kwa
gharama ya Shilingi 18,750,376,421.33
umekamilika
e)
Ujenzi wa kituo cha Mabasi na Malori
Nyamhongolo kwa gharama ya Shilingi 24,197,267,650.77 umekamilika
f)
Ujenzi wa Soko Kuu Mwanza kwa gharama ya Shilingi
26,605,438,559.00 umekamilika
2.5
Utawala Bora na Uboreshaji wa Mazingira ya Kufanyia Kazi
a)
Jumla ya watumishi 4,970 wameajiriwa katika kipindi cha mwaka 2020 –
2025 kwa ajili ya kuboresha huduma kwa
wananchi.
b)
Idadi ya nyumba 6 za wakurugenzi zimejengwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020 – 2025
c)
Idadi ya nyumba 4 za wakuu wa wilaya zimejengwa kuanzia mwaka 2020 – 2025
d)
Idadi ya nyumba 4 za makatibu tawala wa wilaya zimejengwa kuanzia mwaka 2020 –
2025
b)
Idadi ya Ofisi za watendaji wa kata zimeongezeka kutoka ofisi 96 mwaka
2020 hadi ofisi 113 mwaka 2025 sawa na ongezeko la ofisi 17.
c)
Ujenzi wa majengo ya utawala yameongezeka kutoka majengo 2 mwaka 2020
hadi majengo 8 mwaka 2025 sawa na ongezeko la majengo ya utawala 6
d)
Idadi ya nyumba za wakuu wa Idara zimeongezeka kutoka nyumba 5 mwaka
2020 hadi nyumba 24 mwaka 2025 sawa na ongezeko la nyumba 19
e)
Idadi ya magari kwa ajili ya matumizi ya ofisi imeongezeka kutoka magari
147 mwaka 2020 hadi magari 184 mwaka 2025 sawa na ongezeko la magari 37
f) Idadi ya ofisi za maafisa tarafa
zimeongezeka kutoka 3 mwaka 2020
hadi 15 mwaka 2025 sawa na ongezeko la ofisi 12
g) Jumla ya watumishi 25,934 wamepandishwa madaraja
h) Jumla ya watumishi 19,722 wamepandwa Vyeo
i)
Jumla ya watumishi 4,068 wamelipwa madeni yasiyo ya mishahara yenye
thamani ya Shilingi 3,849,275,634.54
HITIMISHO
Mkoa wa Mwanza unaipongeza
sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuleta maendeleo katika Taifa letu. Mkoa
unaahidi kutoa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo ya uchumi ili kuwezesha
kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi. Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza tunamtakia Mhe. Samia Suluhu
Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kheri na baraka katika kusimamia
utendaji wa shughuli za Serikali kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya
haraka.
Comments