ameahidi kujenga tanki kubwa la maji lenye ujazo Lita bilioni moja ili kutatua tatizo la maji katika Kata nne.
Ahadi zingine alizozitoa ni ujenzi wa barabara ya Tabora- Isenga na Ndono - Makazi, fedha za ujenzi wa daraja la Loya tayari fedha zimetengwa na kwamba likikamilika anataka wananchi wapite kwa raha hata wakati wa mvua.
Dkt. Samia ametoa ahadi hizo katika mkutano wa Kampeni uliofanyikw Ilolangulu , Uyui, mkoani Tabora Septemba 11, 2025.
.Aidha, Dkt. Samia amewapongeza wakulima wa Tumbaku kwa kuongeza uzalishaji wa Tumbaku kutokana na Serikali kutoa mbolea ya Ruzuku.
Amewaahidi wakulima wanaodai malipo yao kuwa wavute subira Serikali kupitia Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe yupo kwenye mazungumzo na kampuni mbilli zinazodaiwa muda si mrefu watalipwa.
Amesema tatizo hilo la madeni litapungua kutokana na jitihada za Serikali kuongeza kampuni nyingi za kununua Tumbaku.
Comments