DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA BARABARA YA MZUNGUKO TABORA

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi  kujenga barabara ya mzunguko yenye urefu wa Km. 82 Ili kupunguza msongamano katikati ya Manispaa Tabora.


Amesema kuwa Barbara hiyo itakayotumiwa kupitia malori yanayokwenda mikoa mingine tayari wameifanyia tathmini.


‎Aidha, amesema kuwa endapo wananchi watampatia ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu, ataupendezesha mji huo kwa kuweka taa 2300 Ili kuwawezesha vijana na wananchi kwa ujumla kufanya biashara kwa saa 24, hivyo kupata ajira na kuinua kipato chao.


‎Kwa kuuenzi mkoa huo, wenye hitoria kubwa katika nchi hii hasa kisiasa, Dkt. Samia ameahidi kujenga madaraja 133 katika barabara mbalimbali zinazojengwa kwa gharama ya zaidi ya sh. Trilioni 1.9 mkoani humo.


‎"Mji wa Tabora wenye hitoria kubwa  inabidi iende na vitu vikubwa tunakwenda kujenga madaraja 133 katika barabara tulizoziweka kwenye Ilani, lakini pia tunakwenda kuweka taa 2300 za barabarani,  hivyo Tabora kazi mnayo, mtapata fursa ya kufanya biashara masaa 24 kwa sababu umeme ni usalama na ni mwanga pia."Amesema Dkt. Samia.


Dkt. Samia ametoa ahadi hizo na nyinginezo alipokuwa akijinadi katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Nanenane eneo la Ipuli, Tabora leo Septemba 12, 2025.


Pia, Serikali atakayoiongoza itahakikisha inaendelea kutoa ruzuku katika mbolea na pembejeo pamoja na kuboresha na kujenga miundombinu ya umwagiliaji, kujenga mabwawa ya kunyweshea mifugo, kujenga majosho na kutoa dawa za chanjo.


Aidha, Dkt. Samia amesema akichaguliwa katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025 na kupata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha anakamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu ya maji, afya, elimu,  nishati na mingineyo.


‎Akiwa katika mikutano hiyo, Dkt. Samia huwa anajinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika wilaya hizo, pia kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.


Pamoja na kuelezea kwa undani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho.


Dkt. Samia ambaye kwa Mkoa wa Tabora amehitimisha kampeni zake leo, jana  alifanya kampeni zake Ilolangulu wilayani Uyui, Urambo na Kaliua. Juzi alifanya Igunga na Nzega.


Baada ya uzinduzi wa kampeni kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam Agosti 28, 2025 leo mgombea huyo amemaliza kwa kishindo mkoa wa nane wa Tabora baada ya kufanikisha kwa kiwango cha hali ya juu  kampeni katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa na Singida.


Kesho Septemba 13, 2025 kampeni zake zinaingia katika mkoa wa tisa wa  Kigoma. Kampeni kwa nchi nzima zitafikia tamati Oktoba 28, 2025.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA