KIONGOZI MKUBWA WA ACT- WAZALENDO ATIMKIA CCM, APOKELEWA NA DKT. SAMIA




MRATIBU wa Chama Cha ACT -Wazalendo, Saidi Rashid amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuona matokeo mazuri ya maendeleo mkoani Kigoma yaliyofanywa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rashid ambaye pia amewahi kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini na Mwenyekiti wa ACT wa Mkoa huo, amekabidhi kadi ya chama hicho kwa Dkt.Samia katika mkutano wa kampeni za CCM Kigoma Mjini Septemba 14, 2025.

"Niwaambie, hapa tulipo ni kitovu cha baba, mama na babu yangu hivyo nimeamua kuachana na ACT na kujiunga na CCM mchana kweupe ili nikitumie cha kikubwa chenye mambo makubwa," amesema Rashid na kuongeza kuwa hayupo peke yake, nyuma yake wapo wengi anaohama nao.

Rashidi ambaye ameihama ACT na wenzake 200, amesema kuwa amefurahishwa na matokeo  mazuri na ya muda mfupi yaliyopatikana  mkoani Kigoma yaliyofanywa na Dkt. Samia ambaye ni kiongozi bora wa chama kinachoendeshwa kitaasisi.

Ametaja baadhi ya miradi iliyomfurahisha ni maji, umeme, barabara na ujio wa Treni ya SGR.

Amesema kuwa Dkt. Samia ni kiongozi bora na imara anayeweza hata kuongoza kuwa rais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za Afrika zikiungana.

Baada ya kumpokea, Dkt. Samia amewashukuru wana Kigoma kwa kumzaa kijana wao Said Rashid ambaye amejiunga na CCM na kwamba  kwa hali hiyo CCM itashindwaje Kigoma.Amewaomba wananchi wa Kigoma kuhakikisha Oktoba 29, mwaka huu hawakosi kwenda kuipigia CCM.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA