KISHINDO CHA KIJANI CHA CCM KUTIKISA PEMBA LEO

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutikisa kisiwani Pemba hii leo.
Tayari wananchi wanaendelea kumiminika katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake, Pemba kusikiliza sera imara za chama tawala nchini Tanzania.
Rais Dkt.Samia anatarajia kufanya mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi mkuu hii leo katika uwanja wa Gombani ya Kale kwa ajili ya kunadi Ilani ya uchaguzi ya CCM na kuomba kura kwa wananchi wa Pemba.
Anafanya mkutano huo, baada kufanya mikutano miwili mikubwa yenye mafanikio  katika mikoa ya Kusini Unguja na Kaskazini Unguja, Visiwani  Zanzibar.
Kwa nyakati tofauti, Mgombea huyo wa urais, Rais Dkt. Samia amewasisitiza Watanzania kuhakikisha wanatunza amani, umoja, utulivu na mshikamano wakati wote wa uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu.
Amani ndiyo msingi wa kila kitu, huku akisistiza vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kukabiliana na jambo lolote la uvunjivu.
Aidha, amewasihi wananchi siku ya kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu  kwenda kutimiza wajibu wa kikatiba kisha kurudi nyumbani na kusubiri matokeo.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE