Baadhi ya vijana wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo mama lishe, fundi mchundo, wauza viatu vya mtumba na bodaboda wa Songea mjini, Mkoa wa Ruvuma, wakielezea kufurahishwa na utendaji mzuri wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea maaendeleo makubwa ikiwemo ujenzi wa barabara, hospitali, shule na utoaji mikopo isiyo na riba.
Kwa mambo makubwa yaliyofanywa na Dkt. Samia Songea na Mkoa mzima wa Ruvuma, vijana hao niliofanya nao mahojiano leo Septemba 20, 2025, wameahidi kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2025.
Dkt. Samia anatarajia kuingia Mkoa wa Ruvuma kesho Septemba 21, 2025 na kujumuika pamoja na Mgombea Mwenza ambaye ni mzawa wa mkoa huo, Dkt. Emmanuel Nchimbi katika mikutano ya kampeni mkoani humo.
Mama Lishe Shani Baraka.
Muuza viatu Charles Yusufu.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments