Muendelezo wa mchakamchaka wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa njiani kutokea Mkoani Iringa kuelekea Jijini Dodoma.
HODIII SINGIDAAA
Kishindo cha kijani cha Chama Cha Mapinduzi kutikisa kesho mkoani Singida.
Kishindo hicho kinajiri wakati Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, atakapowasili Mkoani humo akitokea mkoani Dodoma.
Hii ni mwendelezo wa mikutano ya kampeni ili kuomba ridhaa ya watanzania kushika dola.
Akiwa njiani kuelekea mkoa wa Singida Rais Dkt.Samia atakuwa na mkutano jimbo la Bahi Mkoani Dodoma.
Ndani ya mkoa wa Singida, atafanya mikutano Manyoni, Ikungi na kisha mkutano mkubwa Singida Mjini katika uwanja wa Bombadia.
Mpaka sasa historia anayotembea nayo Rais Dkt.Samia ni idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kumsikiliza akinadi Sera na Ilani ya uchaguzi ya Chama chake akiwa amebeba kauli mbiu ya Kazi na Utu,Tunasonga Mbele.
Comments