NMB Yakabidhi Jezi za Milioni 36 kwa Shimiwi

Benki ya NMB imekabidhi jezi zenye thamani ya Shilingi milioni 36 kwa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kukuza michezo miongoni mwa watumishi wa umma nchini.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa Shimiwi wakiongozwa na Katibu Mkuu Alex Temba na Naibu Katibu Mkuu Mariam Kihange. Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano ya Benki ya NMB na Serikali, Amanda Feruzi, alisema benki inaona michezo kama chachu ya mshikamano, afya bora na kuongeza ari ya utendaji kazi kwa watumishi.

Katika makabidhiano hayo, NMB ilikabidhi jezi, tracksuit na kombe kwa uongozi wa Shimiwi, ikiwa ni maandalizi ya michezo inayowakutanisha Wizara na Idara za Serikali. Viongozi wa NMB walioungana na Feruzi katika tukio hilo ni Meneja NMB Kenyatta Deogratius Kawoga na Meneja Mahusiano Mwandamizi wa NMB, Josephine Kulwa.

Katibu Mkuu wa Shimiwi, Alex Temba, alishukuru NMB kwa msaada huo akibainisha kuwa utasaidia kuimarisha maandalizi ya timu na kuongeza hamasa kwa washiriki wote wa michezo ya Shimiwi. Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya taasisi za kifedha na mashirikisho ya michezo unatoa mchango mkubwa katika kukuza vipaji na mshikamano wa kijamii.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE