RUVUMA WAMHAKIKISHIA USHINDI WA KISHINDO DKT. SAMIA

 

Na Richard Mwaikenda, Mbinga
MKOA wa Ruvuma umemhakikishia ushindi wa kishindo, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.


Ahadi hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Doyo Mwisho alipokaribishwa kutoa neno katika mkutano wa Kampeni za CCM wilayani Mbinga leo Septemba 21,2025.


"Ndugu Mwenyekiti mimi sina maneno mengi, hawa wagombea ubunge umewasikia na hawa wanachama na wananchi ni  mashuhuda, nimepanga vikosi vya ushindi vya Oktoba 29," amesema kwa kujiamini, Mwenyekiti Doyo na kuongeza...


Kazi moja ni ushindi na tumehakikisha na kumthibitishia  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, dada yetu, Laila Ngozi Mratibu wa Mkoa wetu, kwamba Ruvuma tunachukua namba moja, na hayo ni ndiyo maazimio yetu na ndiyo maana mara nyingi nasema maneno kidogo kazi zaidi," amesisitiza Doyo huku akiitikiwa na wananchi waliofurika katika mkutano huo.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE