Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Singida katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho zilizofanyika katika uwanja wa Bombadia mkoani Singida tarehe 09 Septemba, 2025.
Pamoja na mambo mengine, Dkt.Samia amewaahidi wakazi wa Mkoa wa Singida kuwatafutia soko la mazao ya jamii ya mikunde ambayo ni dengu na mbaazi ili wakulima hao waweze kunufaika na zao hilo kwa kuuza bei yenye faida.
Dkt. Samia amesema serikali ipo kwenye mazungumzo na serikali ya India ili kutafuta soko hilo ambapo amewahakikishia wakulima kuwa makubaliano yatakayofanyika hayatoshuka chini ya asilimia 60 ya soko la dunia.
> Vilevile, amewaasa wakulima hao kutokuuza mazao hayo akiwaahidi hivi karibuni serikali ina mpango wa kutoa vibali kwa wafanyabishara kusafirisha mazao hayo nje ya nchi.
> Dkt. Samia amesema hayo leo Septemba, 2025 mkoani Singida wakati wa mkutano wake wa kampeni

Nishangwe kwa kwenda mbele.
Comments