Amesema kuwa watu watakuwa wanajiuliza fedha zitapatikana wapi, ila yeye na Mchemba wanajua watazipata wapi Ili kufanikisha jambo hili muhimu kwa maisha ya watu.
Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo alipokuwa akijinadi katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa CCM Lulumba Makao Makuu ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida Septemba 10, 2025.
Amesema kuwa kwa uwingi wa watu waliojitokeza kwenye mkutano huo ana uhakika Iramba watalamba kura nyingi zitakazomwezesha kuongoza tena Nchi na kufanikisha mradi huo muhimu.
Ametaja miradi mingine watakayoipa kipaumbele ni; ujenzi wa umeme wa upepo, kukamilisha utafiti wa uzalishaji wa mafuta ziwa Eyasi pamoja na kukamilisha mazungumzo na Serikali ya India kuhusu ununuzi wa mazao ya dengu, mbaazi na ufuta kwa bei ya kuridhisha.
Aidha, Dkt. Samia amesema akichaguliwa katika Mkutano Mkuu Oktoba 29, 2025 na kupata ridhaa ya kuongoza Nchi atahakikisha anakamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu ya barabara, maji, afya, elimu, nishati na mingineyo.
Akiwa katika mikutano hiyo, Dkt. Samia anajinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika wilaya hizo, pia kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Pamoja na kuelezea kwa undani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. Emmauel Nchimbi, ametumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho. Jana amefanya kampeni katika Mji wa Manyoni, Ikungi na Singida Mjini.
Baada ya uzinduzi wa kampeni kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam, leo Mgombea huyo ameingia kwa kishindo mkoa wa Nane wa Tabora baada ya kufanikisha kwa kiwango cha hali ya juu kampeni katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa na Singida.
Comments