MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa mwito kwa wananchi kutokukubali kuchokozeka na wanaotamani kuvuruga amani na uchaguzi.
Amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupigakura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025 na kwamba hakutakuwa na vurugu kwani vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kulinda amani.
Akihutubia maelfu ya wananchi wa Visiwa Zanzibar leo Septemba 20,2025 katika Viwanja vya Gombani ya Kale Mkoa wa Kusini Pemba Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kuendelea kuwahakikishia wananchi uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu.
“Katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, wapo baadhi ya watu wanatamani kuvuruga amani, hivyo nitoe mwito kwa wananchi kutokubali kuchokozeka.
“Lakini niwahakikishie Oktoba 29 mwaka hakutakuwa na vurugu zozote .Wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kutimiza takwa la kidemokrasia kuchagua viongozi wanaowataka.Msichokozeke, kuweni kama mimi mama yenu, dada yenu na bibi yenu.
“Mimi ninachokozeka sana lakini sikubali kuchokozeka. Tusiende kuvunja amani ya nchi, tutunze amani na utulivu. Tunapochokozwa tusichokozeke.
“Tarehe 29 hakutakuwa na vurugu, vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kulinda nchi na ninayezungumza hapa ni Amiri Jeshi Mkuu,”amesema Dk.Samia alipokuwa akizungumza kuhusu umuhimu wa kulinda amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu.
Amesisitiza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali imejitahidi kusimamia utulivu wa kisiasa na amani ambapo hakuna vurugu zozote zilizosikika."Wenzetu wanayolalamikia hakuna lisilozungumzika.”
“Tutakaa tutazungumza, tusiende kuleta vurugu kuvunja amani kwa sababu hili halikufanyika. Tukapige kura, turudi nyumbani tusubiri matokeo," amesema mgombea Urais Dk.Samia .
Pamoja na hayo Dk.Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Serikali za CCM ni vitendo na siyo maneno na ndio maana yote yaliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020-2025 yametekelezwa na maendeleo yanaonekana katika sekta mbalimbali.
“Pemba kila kukicha imekuwa ikibadilika ikiwa ni matokeo ya miradi ya maendeleo inayoletwa kisiwani hapa.Serikali za CCM zinafanyakazi kwa vitendo na siyo blah..blah...kila nikija Pemba mambo yanaendelea kubadilika,”amesema Dk.Samia alipokuwa akizungumza na wananchi hao akihitimisha mikutano yake ya kampeni Zanzibar.
Ametaja baadhi ya miradi mikubwa inayotekelezwa ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba ambao utakuwa wenye hadhi ya kimataifa huku akifafanua uwanja huo baada ya kukamilika ndege kubwa za abiria na mizigo zitatua, hivyo kufungua zaidi uchumi.“Watalii na ndege za mizigo watafika moja kwa moja Pemba badala ya kutua unguja.”
Aidha amesema miradi mingine ni ujenzi wa barabara ya Chake chake - Mkoani ambao fedha zake zimeshapatikana.”Ujenzi wa Bandari ya Shumba utarahisisha shughuli za uchukuzi baina ya Pemba na Mombasa hatua ambayo itaondoa changamoto ya usafiri.”
Ameongeza kwamba wakazi wa maeneo hayo watatumia boti za kisasa badala ya usafiri wa vidau ambavyo usalama wake ni mdogo.Amesema kisiwa hicho kimenufaika kupitia ujenzi wa shule za ghorofa ikiwemo eneo la Kojani.
Akieleza zaidi Dk.Samia Suluhu Hassan kutokana na maendeleo makubwa yaliyopatikana ndio maana wanaoujasiri wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena.
“Tunaamini tumeweza kufanya makubwa, makubwa mengine zaidi tunaweza kuyafanya. Tupeni mitano mingine tufanye makubwa zaidi. Tunafanyakazi kustawisha maisha ya wananchi. Mtu akifanyakazi ipasavyo atapata ujira kisha kufanya maendeleo. Kazi na Utu maana yake ni kusonga mbele.”
HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI
NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE
Alhamdulillah ala kulli hal Nimepokea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa moyo wa shukrani. Quran Tukufu inatufundisha kuwa Allah ndie mpangaji na ni bora kwetu. ALHAMDULILLAH Ndugu zangu wanaTanga Mjini, nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuniamini kuwa Mbunge wenu kwa kipindi cha miaka 5 (2020 - 2025) Nafurahi kuona kuwa utumishi wangu kwenu umewagusa wengi na umeacha alama kubwa za kimaendeleo katika Jimbo letu. Asanteni kwa ushirikiano mzuri mlionipatia ktk kipindi chote cha Utumishi wangu. Kwa dhati ya moyo wangu, ninawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Tanga kwa kunipa kura nyingi ktk mchakato wa kura za maoni za kutafuta mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo letu Tanga Mjini kwa kipindi cha 2025 - 2030. Mlinikopesha imani kubwa sana Nitaienzi na kuithamini imani hii daima. UAMUZI wa vikao vya Chama ni lazima UHESHIMIWE. Nampongeza Ndugu Kassim Amar Mbaraka (Makubel) kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM Tanga Mjini. Ninawaomba wanakimji wen...
WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI
1. Ummy Mwalimu - Tanga. 2. Stanslaus Mabula - Nyamagana 3. Shaban Mrutu - Tabora Mjini 4. Malecela - Dodoma. 5. Luqman Merhab - Mufindi Kastazini 6. Kirumbe Ng' enda - Kigoma. 7. Alexander Mnyeti - Misungwi 8. Prof Edwinius Lyalya - Magu. 9. Robert Maboto - Bunda. 10. Fredrick Lowassa - Monduli. 11. Munde Tambwe - Sikonge
MTOKO MPYA WA YANGA HUU HAPA
KILUNBE NG'ENDA ATEULIWA KUWA NAIBU KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI CCM
𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗔𝗠𝗘𝗪𝗔𝗝𝗘𝗡𝗚𝗘𝗔 𝗪𝗔𝗡𝗔𝗪𝗔𝗞𝗘 𝗠𝗢𝗬𝗢 𝗪𝗔 𝗨𝗝𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜 𝗡𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗔𝗠𝗜𝗡𝗜 𝘼𝙢𝙚𝙚𝙡𝙚𝙯𝙖 𝙆𝙖𝙩𝙞𝙗𝙪 𝙈𝙠𝙪𝙪 𝙢𝙨𝙩𝙖𝙖𝙛𝙪 𝙬𝙖 𝘾𝘾𝙈, 𝘿𝙠𝙩. 𝘽𝙖𝙨𝙝𝙞𝙧𝙪 𝘼𝙡𝙡𝙮 "Kwa muda mrefu katika historia ya siasa Duniani kote, nafasi ya mwanamke imekuwa nafasi ya pili kanakwamba utu wake ni nusu..duniani kote ajenda ya kuweka usawa kwa wanaume na wanawake imekuwa mfupa mgumu.." "..CCM kwasababu ya msimamo wetu wa kifalsafa na kiitikadi, usawa wa wanaume na wanawake si suala la hiari ni saula la lazima.." "..katika uongozi wako Rais Dkt. Samia...kitakwimu katika kipindi ulichoingia kama Mkuu wa nchi na Mwenyekiti wa chama (CCM) , kitakwimu angalieni maamuzi, sera, miradi na namna utekelezaji wake ulivyoinua hali za akina Mama.." Dkt. Bashiru ameyasema hayo leo tarehe 9 Septemba 2025 wakati akizungumza na maelfu ya Wananchi wa Singida Mjini waliojitokeza katika uwanja wa Bombadia kumlaki na kumsikiliza Mgombea...
CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-
"Miaka 12 iliyopita nilipata fursa ya kujifunza diplomasia na ustahimilivu kupitia aliyekuwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa [SUKI] Dr. AshaRose Migiro. Alinitaka muda wote kutenda kwa kuandaa maandiko na kuyasaili kisha ndipo nitende. Shule ile ilinikaa na kunifanya muda wote nikikutana naye hata baada ya kuhama ofisi moja na nyingine nimkumbuke kama mwalimu imara. Miaka imeenda na siku zikasonga mbele." "Leo ameaminiwa kushika nafasi ya juu ya utendaji ya CCM. Nafasi ambayo nami nilishaitumikia kabla ya mtangulizi wake. Hakika nimefurahi kuona Mwalimu akikabidhiwa darasa kufundisha. Kazi muhimu ni wanafunzi kubeba utayari. Karibu tena nyumban SG mpya." "Sisi tupo tayari kutumwa. Picha hii ni kumbukumbu ya mimi na SG mpya katika mkutano Mkuu uliopita." #KaziNaUtuTunasongaMbele #NaendeleaKujifunza
MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA
*1. Usiweke Akiba Mwishoni Weka Mwanzoni* Watu wengi wanasubiri walipwe mishahara au kupata faida ndipo waanze “kuona kama kimebaki” ili waweke akiba. Hii ni kosa.. Weka akiba mara tu unapopokea kipato (10%–20% ya mapato yako). *2.Usitumie Pesa Yote Jifunze Kuishi Chini ya Kipato* Ukiwa na kipato cha 1M, usipange matumizi ya 1M. Panga matumizi ya 700k–800k. Unapojilazimisha kuishi chini ya kipato chako, unajilinda dhidi ya dharura na kuacha nafasi ya kuwekeza. *3.Kuwa na Vyanzo Zaidi ya Kimoja cha Mapato* Hata ukiwa na kazi nzuri, biashara ndogo au uwekezaji mdogo ni ngao ya kifedha. Mfano: Mwalimu mwenye mshahara anaweza kuwa na shamba la nyanya au kuuza mtandaoni. *4.Epuka Madeni Mabaya* Kuna madeni mazuri (yanayokuongezea kipato, kama mkopo wa mashine ya biashara) na mabaya (kukopa kwenda kwenye sherehe au kununua simu ya anasa) Deni baya ndilo chanzo kikuu cha watu kuishiwa pesa kila wakati *5.Wekeza Badala ya Kuweka tu Akiba* Akiba inalinda lakin...
DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO
Karibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha Rose Migiro akiungana na vijana wa CCM katika amsha amsha katika mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan mjini Makambo Njombe asubuhi hii ya Septemba 6, 2025. BAADA ya kumaliza Kampeni katika Mikoa wa Njombe,leo anaingia mkoani Iringa.
WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE
Watetezi wa majimbo yao walioanguka 1. Stela Manyanya (Nyasa) 2. Emmanuel Mwakasaka (Tabora Mjini) 3. Charles Kimei (Vunjo) 4. Deo Sanga (Makambako) 5. Antipas (Malinyi) 6. Nagindu Butondo (Kishapu) 7. Joseph Kakunda, (Skonge) 8. Ally Makoa (Kondoa Mjini) 9. Mwarami, 10. Amsabi Mrimi (Serengeti) 11. Benaya Kapinga (Mbinga) 12. Issa Chinguile (Nachingwea) 13. Doroth Kilave (Temeke) 14. Issa Mtemvu (Kibamba) 15. Hassan Mtenga (Mtwara Mjini), 16. Isack Francis Mtinga (Iramba Mashariki) 17. Innocent Bilakwate - Kyerwa 18. Assa Makanika (Kigoma Kaskazini) 19. Vita Kawawa (Namtumbo) 20. Jesca Msambatavangu (Iringa Mjini) 21. Anania Thadayo (Mwanga) 22. Atupele Mwakibete (Busekelo) 23. Joseph Ndaisaba (Ngara) 24. Cosato Chumi (Mafinga) 25. Joseph Kizito Mhagama (Madaba) 26. Maimuna Mtanda (Newala V) 27. Stanslaus Nyongo (Maswa Mashariki) 28. Marco John Sallu (Handeni Mjini) 29. Dkt. Daniel Pallangyo (Arumeru Mashariki) 31. Prof. Patrick Ndakidemi (Moshi Vijijini) 32. Exhaud K...
Comments