𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗘𝗡𝗚𝗔 𝗠𝗔𝗚𝗛𝗔𝗟𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗛𝗜𝗙𝗔𝗗𝗛𝗜𝗔 𝗠𝗔𝗭𝗔𝗢

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 akizungumza na maelfu ya wananchi wa Masumbwe wilayani Mbogwe, ametoa ahadi kuwa iwapo watanzania wataendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi na kuchaguliwa kupata ridhaa ya kuunda serikali kwa miaka mitano ijayo, Serikali yake anayoiongoza itajenga maghala ya kuhifadhia mazao pamoja na soko la kisasa wilayani Mbogwe mkoani Geita ili kusisimua biashara na kilimo mkoani humo.

Akizungumzia katika kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara mkoani humo, Dkt. Samia ameahidi kuanza ujenzi wa barabara ya Masumbwe- Kasosobe, kuelekea Makao makuu ya wilaya hiyo, barabara yenye urefu wa Kilomita 45 itakayojengwa kwa kiwango cha lami ili kuondoa adha ya usafiri na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.

Pia, Dkt. Samia amesisitiza mpango wake wa kuendelea kutoa huduma za kijamii kwa kila mwananchi ikiwemo huduma za afya, elimu, maji na nishati huku akisema kazi hiyo ni kazi endelevu na itafanyila kila awamu ya serikali ili kutoa huduma za uhakika na zenye viwango kwa kila mwananchi wa Tanzania.

Aidha, Dkt. Samia ametoa salamu zake za shukrani kwa wananchi hao kuonesha upendo mkubwa wa kuja kumlaki na kumsikiliza ambapo pia ametoa wito wa kuwataka kushiriki uchaguzi kikamilifu na kwenda kuendeleza imani yao ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi huku akisisitiza kuwa  "tupeni kazi tukaifanye kazi ya kuleta maendeleo endelevu na kuinua utu wa kila mtanzania"

Dkt. Samia ameanza mikutano yake leo Oktoba 12, 2025 ndani ya mkoa wa Geita katika kuendelea kuinadi ilani ya CCM (2025/30) Sera na Ahadi zake.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM

DKT. SAMIA AWASILI ZANZIBAR

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA