DKT. SAMIA APONGEZWA KUOKOA ZAIDI YA WASICHANA 1OOO WALIOPATA MIMBA SHULENI


 MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa ameokoa zaidi ya wasichana wa kike 1000 waliokuwa shule lakini walikuwa wanashindwa kuendelea na masomo kupata mimba ama kuolewa katika umri mdogo.


"Mamaangu kazi uliyoifanya inawezeksna Kuna mwanamke anaweza kusimama akabeza wewe kuwa Mgombea uraisi, lakini nakuhakikishia hilo jambo rahisi, mwaka 2021 ulivyoingia madarakani katika wasichana 1000 waliodahiliwa waliacha shule kwa sababu ya kupata mimba na kutoa mimba."


...Leo tunazungumza miaka mitatu kati ya wasichana 1400 waliodahiliwa ni 400 tu walioshindwa kwenda shule, umeokoa zaidi ya wasichana 1000 akina Mama Samia wengine katika Taifa hili,hongera umefanya Kazi kubwa Mama."


Wengi wao wamemaliza vyema masomo yao na kupata Kazi wanasaidia kusukuma kurudumu la maendeleo ya Taifa.


Pongezi hizo zimetolewa na Salome Makamba Mbunge mstaafu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alipokaribishwa kutoa salamu katika  mkutano wa Kampeni za Dkt. Samia kwenye Uwanja wa Magufuli Kahama Mjini mkoani Shinyanga Oktoba 11, 2025. Makamba  amejiunga CCM

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM

DKT. SAMIA AWASILI ZANZIBAR

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA