MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameendelea kuchanja mbuga kwa ajili ya kuomba kura za mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Leo Oktoba 14,2029 Dk.Nchimbi anafikia mkoa wa 23, akifanya mkutano mkubwa wa kampeni katika Uwanja wa CCM uliopo Kata ya Ilongero, jimbo la Ilongero katika Wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida.
Akiwa katika mkutano huo Dkt.Nchimbi ameendelea kumuombea kura Mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili ashinde kwa kishindo, kuomba kura za wabunge na madiwani.
Mbali ya kuomba kura za wagombea wa CCM, pia akiwa katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jimbo hilo pia ametumia nafasi hiyo kunadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030.
Wakati huo huo Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ilongero, Ndugu Haidary Gulamali na Madiwani.
Comments