LICHA ya Taifa Stars kupoteza kwa bao 2-1 dhidi ya Nigeria, beki wa Stars, Ibrahim Bacca ameonesha kiwango cha juu kwa kumdhibiti vyema mshambuliaji hatari wa Nigeria na klabu ya Galatasaray, Victor Osimhen.
Katika mchezo huo, Osimhen alionekana kukosa nafasi nyingi alizotarajia, huku akionesha dalili za kutofurahia kufanyiwa mabadiliko kabla ya kumalizika kwa dakika 90 bila mafanikio yoyote mbele ya lango la Stars.
Ulinzi wa Taifa Stars ulisimama imara kwa nyakati nyingi, jambo linaloonesha maendeleo makubwa ya timu licha ya matokeo.
Vipi wewe mdau wa soka, umeonaje kiwango cha Taifa Stars katika mchezo huu?
Timu ya Taifa ya Tanzania imepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nigeria kwa bao 2-1 katika mashindano ya AFCON 2025 yanayofanyika Nchini Morocco.
Katika mchezo huo Nigeria walikuwa wakwanza kupata goli kupitia kwa Beki wao wa kati mnamo dakika ya 36 Semi Ajayi, Stars ikasawazisha bao Hilo dakika ya 50 ya mchezo kupitia Charles M'mombwa, dakika ya 52 Adebora Lookman akaiandikia Nigeria bao la 2 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 2-1.

Comments