Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais Mteule wa Uganda, Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo.
Katika ujumbe wake, Rais Samia amesema ushindi wa Rais Museveni unaakisi imani na dhamana kubwa ambayo wananchi wa Uganda wanaendelea kuwa nayo kwake, huku akiahidi kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo kwa maslahi ya wananchi.

Comments