Safari ya YANGA kwenye michuano ya CAF kwa kipindi cha miaka 5 (2020/21 hadi msimu huu 2024/25) ni kama ifuatavyo.
MWAKA 2020/21.
Yanga haikushiriki kabisa michuano ya CAF kwani kwenye klabu bingwa alishiriki simba huku shirikisho walishiriki Namungo Fc, hivyo YANGA haikupata point yoyote (0×1)= 0.
MWAKA 2021/22.
Yanga walitolewa hatua za awali kabisa na Rivers united ya Nigeria hivyo kwa sababu hawakufika makundi maana yake hawakupata point yoyote (0×2)= 0.
MWAKA 2022/23.
Yanga walifika hatua ya Fainal kombe la shirikisho na kufungwa na USM Alger hivyo walikua washindi wa pili (runner-up) na walikusanya points 4 ambazo zinazidishwa kwa 3 kwa sababu ni mwaka wa 3 kimahesabu (4×3)= 12.
MWAKA 2023/24.
Yanga walifika Robo fainal ya klabu bingwa na kutolewa na Mamelod sundown hivyo kwa kufika hatua hiyo walikusanya points 3 ambazo zinazidishwa kwa 4 kwa sababu ni mwaka wa nne kimahesabu (3×4)= 12.
MWAKA 2024/25 mpaka sasa yanga wana uhakika wa points mbili (2x5=10) lakini wakifuzu kwenda Robo Fainal zitaongezeka na kua points 3 ambazo zinazidishwa kwa tano (3x5=15).
Kabla ya Kufuzu Robo Fainali points za yanga mpaka sasa ni 34 (0+0+12+12+10=34), hivyo Yanga watasalia na points 34 endapo hawatatinga hatua ya Robo Fainali.
Endapo watatinga Robo Fainal mahesabu yatakua kama ifuatvyo (0+0+12+12+15=39), ponts ambazo zitaipeleka Yanga hadi nafasi ya 5 na kuishusha waydad Casablanca .
Jiunge na group letu la Whtsapp
https://chat.whatsapp.com/BXMQWuu71esFNiiOvSFsf1
MUNGU IBARIKI YANGA SC 🙏🙏

Comments