Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewatuhumu baadhi ya wanaharakati kulipwa fedha ili kuichafua taswira ya Tanzania kimataifa kwa lengo la kuhujumu sekta ya utalii na kupotosha dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma Januari 17, 2026, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amesema kuna njama zinazofanywa na watu wanaojiita wanaharakati kwa kushirikiana na baadhi ya wanasiasa kuhamasisha watalii wasije nchini, jambo ambalo ameliita ni "uangamizaji wa uchumi wa mwananchi wa kawaida."
Kihongosi amefafanua mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii ambao unajumuisha madereva, waongoza watalii (tour guides), wamiliki wa hoteli, wafanyakazi, na wakulima wanaouza mboga na mayai kwenye mahoteli, akisema hatua yoyote ya kuichafua nchi nje ya mipaka inaenda kukata vipato vya familia hizi za Kitanzania.
Comments