AKWILAPO AONGOZA MAWAZIRI KIKAO CHA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MASHAMBA YA UWEKEZAJI MUHEZA

Na Munir Shemweta, WANMM MUHEZA

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Leonard Akwilapo amewaongoza Mawaziri wenzake wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Ofisi ya Raisi Mipango na Uwekezaji katika kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.

 

Kikao hicho kimefanyika tarehe 18 Februari 2026 katika ofisi ya Mkuu wa wilaya Muheza mkoa wa Tanga ikiwa ni utekelezaji wa masuala yaliyojitokeza wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba.

 

Mawaziri hao ni Prof. Riziki Shemdoe, Waziri wa TAMISEMI na Dkt. Pius Chaya, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji ambao kupitia kikao hicho, kilichohusisha pia wataalamu, viongozi hao walipata fursa ya kuwahoji wananchi walioguswa na migogoro hiyo ya mashamba ya uwekezaji ambayo yaliyofutiwa umiliki mwaka 2016.

 

Mashamba hayo ni Azimio/ Kilapula Geiglitz, Bwembwera, Kibaranga, Kihuhwi, Lewa pamoja na Saguras yaliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Wa pili kushoto ni Waziri wa TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe na kulia ni Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji Dkt. Pius Chaya na Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Ayubu Sebabili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe (Wa pili kushoto) akizungumza katika kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Dkt. Jumaa Mhina akizungumza wakati wa kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Dkt. Pius Chaya (Kulia) akisisitiza jambo wakati kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji kwenye wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian.


Baadhi ya wananchi walioguswa na mgogoro wa mashamba ya uwekezaji katika halmashauri ya Muheza mkoa wa Tanga wakielezea umiliki wao wa maeneo kwenye mashamba hayo mbele ya mawaziri wakati wa kikao cha kujadili utatuzi wa migogoro ya mashamba ya uwekezaji tarehe 18 Februari 2026. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO