Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) kupitia kikao cha Baraza Kuu la UWT kilichoketi leo Februari 14, 2026, katika ukumbi wa NEC jijini Dodoma, ametoa tuzo ya pongezi kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Asha-Rose Migiro kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza toka kuzaliwa kwa CCM, kwa nafasi hiyo kuongozwa na Mwanamke jambo ambalo ni historia katika medani za siasa ndani ya CCM.
Mary Chatanda akikabidhi tuzo hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa UAT, Zainabu Shomari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Migiro.
Comments