DKT. MATARAGIO: PURA ONGEZENI KASI UTAFITI WA MAENEO MAPYA YA MAFUTA NA GESI

 Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kuongeza kasi ya utafiti wa awali katika maeneo mapya ya mafuta na gesi asilia ili kuvutia wawekezaji na kuongeza mapato ya taifa.

Akizungumza leo Februari 26, 2026, wakati wa Mkutano wa Tano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Morogoro, Dkt. Mataragio amesema juhudi hizo zitachochea uwekezaji, kupanua ushiriki wa wazawa na kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya msingi ya taasisi hiyo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa PURA kuendelea kutambua na kuendeleza maeneo mapya ya miradi, kuyatangaza kwa wawekezaji pamoja na kusimamia kikamilifu majukumu yake kama yalivyoainishwa katika malengo ya kuanzishwa kwake.

Miongoni mwa majukumu hayo ni kusimamia na kufuatilia shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia kwa kuzingatia sheria na taratibu, kuishauri Serikali kuhusu masuala ya mkondo wa juu wa mafuta na gesi, pamoja na kutangaza vitalu vilivyowazi kwa ajili ya uwekezaji ili kuongeza ugunduzi wa rasilimali hizo nchini.

Dkt. Mataragio amesema hatua hizo zitasaidia kuongeza mchango wa sekta ya mafuta na gesi katika ukuaji wa uchumi wa taifa na kuimarisha usimamizi wa rasilimali kwa manufaa ya Watanzania.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

MAJESHI YA URUSI CHINA NA IRANI YAANZA MAZOEZI YA PAMOJA DHIDI YA MAREKANI

30 TANZANIAN PROJECTS IN THE NEXT 10 YEARS