Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule (katikati) ametoa msaada wa vyakula, vinywaji, vifaa vya usafi na vyandarua 100 kwa Shule ya Viziwi Dodoma, katika tukio lililofanyika Februari 21, 2026 katika shule hiyo iliyopo Kisasa jijini Dodoma. Katika tukio hilo, Dkt. Majule ambaye yupo mstari wa mbele kujitotea kwa hali na mali katika masuala ya kijamii na hasa kwa watu wenye uhitaji maalumu, alitoa mchele, unga, mafuta, sukari, vinywaji, sabuni, fagio, kalamu, madaftari na pedi kwa ajili ya mabinti. Kabla ya makabidhiano ya msaada huo, Dkt. Majule alipata wasaa wa kutembelea na kujionea jinsi wanafunzi wanavyopata mafunzo kwa njia ya vitendo ikiwemo ushonaji, kompyuta, ufundi umeme na uselemala lakini pia mchezo wa pooltable. Mkuu wa shule hiyo, Awadhi Mbogo alitoa shukrani kwa kitendo cha mbunge huyo kuamua kutoa msaada huo mkubwa kwa shule hiyo na kwa aendelee na moy...
Comments