HUYU NDIYE RASHID MFAUME KAWAWA...

Kubwa 10 kuhusu Rashid Mfaume Kawawa (May 27, 1926 – December 31, 2009)

1. Kawawa alikutana na Nyerere wakiwa wanafunzi Shule ya Tabora Boys.

2. Kawawa alimgomea baba yake mzazi kuendelea na masomo Chuo Kikuu cha Makerere Uganda, na kumshauri Baba yake hiyo pesa asomeshee wadogo zake.

3. Alikuwa Waziri Mkuu mara mbili, Waziri Mkuu Tanganyika 1962 baada ya Nyerere kujiuzulu, akawa tena Waziri Mkuu wa Tanzania 1972 - 1977.

4. Kawawa alishawahi kuwa Waziri wa Ulinzi 1977 - 1980.

5. Wakati Nyerere anang'atuka madarakani 1985, majina matatu yalipendekezwa kugombea, Kawawa, Ally Hassan Mwinyi na Salim Ahmed Salim mmoja apitishwe kugombea urais wa Tanzania. Kawawa aliomba kutolewa kwenye mchakato wa kinyang'anyiro kwani umri wake umeenda na angependa damu changa zaidi ipewe nafasi. Mpambano ukabakia kati ya Ally Hassan Mwinyi na Salim Ahmed Salim, Mwinyi akapitishwa kugombea akawa Rais.

6. 1964 Kawawa alikuwa Makamu wa Rais wa Pili wa Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

7. Kawawa ana shahada mbili ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha Makerere Uganda na Chuo Kikuu cha Dodoma ambazo zote alizipewa wakati ameshafariki.

8. Kawawa alikuwa mnazi mkubwa wa sera za kijamaa kwenye kuendesha uchumi, haishangazi kuona waliiva sana na Mwalimu.

9. Tarehe 27 February 2017 Serikali ilifungua makumbusho maalumu wilayani Songea kumuenzi. Makumbusho hayo yapo Mtaa wa Kawawa, Bombambili Songea Mkoani Ruvuma.

10. Ukiacha siasa, Kawawa anashikilia rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuwa msimamizi wa kuandaa filamu (Director), mwaka 1951 alisimamia filamu ilyoitwa 'Muhogo Mchungu', pia alikuwa mwandika mswada ya filamu (scriptwritter).



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

30 TANZANIAN PROJECTS IN THE NEXT 10 YEARS

MAJESHI YA URUSI CHINA NA IRANI YAANZA MAZOEZI YA PAMOJA DHIDI YA MAREKANI