Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Bw. Martin Chungong amewasili nchini usiku wa kuamkia leo Februari 27, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya kushiriki hafla ya Uwekaji Saini Mkataba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) utakaofanyika Oktoba 2026 Jijini Arusha.
Hafla hiyo ya uwekaji saini inafanyika leo Februari 27, 2026 katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam ambapo Bw. Chungong na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu wataweka saini mkataba huo.



Comments