Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) Imezuia utoaji tuzo wa zabuni 43 zenye thamani ya kiasi cha TZS. 586,502,801,992/= kwa wazabuni waliokosa uwezo wa kifedha na sifa za kitaalamu zinazohitajika kutekeleza zabuni husika.
Hilo limebainishwa na Katibu Mtendaji wa Mamlaka hiyo, alipokuwa akikelezea mafanikio ya Taasisi hiyo katika mkutano na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mji wa Kiserikali, jijini Dodoma Februari 25, 2026.
Hatua hii imezuia utekelezaji usioridhisha wa miradi, ambao ungesababisha upotevu wa fedha za umma na kuchelewesha maendeleo endelevu na stahiki kwa wananchi.
Aidha, katika baadhi ya mashauri hayo, Mamlaka ya Rufani kupitia Sehemu
ya Rufaa (Appeal Schedule) imefanikiwa kusajili mashauri
takriban 196 yaliyotokana na michakato mbalimbali ya
ununuzi wa umma ambayo baadhi ya hayo yamezuiwa.
Serikali ya Awamu ya Serikali ya Awamu ya Sita
inaamini kuwa usuluhishi wa migogoro hauwezi kufanikishwa
katika mazingira ya ubaguzi wala pale ambapo fursa na haki
za kiuchumi na kiraia hazitolewi kwa usawa.
Kwa hivyo,
hatua ya Mamlaka ya Rufani kuzuia utoaji wa tuzo kwa
wazabuni 43 waliokosa sifa za kutekeleza zabuni, inaimarisha
mchakato wa usuluhishi wa migogoro – moja ya falsafa nne
5
(4) za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
mwaka 2023 Serikali ilitunga
upya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, ikifuatiwa
na Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 202
4 pamoja na Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2025. Maboresho haya yameimarisha na kuleta ufanisi katika sekta ya Ununuzi na Ugavi kwa kuunganisha maeneo mengine ambayo kiutaalamu yanapaswa kuwa pamoja. Hapa ninazungumzia dhana nzima ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi (Supply Chain Management). Hii inahakikisha mnyoro mzima wa ugavi unasimamiwa kwa ufanisi, kuanzia upatikanaji wa bidhaa na huduma hadi usambazaji wa mwisho.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments