Tangu Patrice Motsepe achaguliwe kuwa raisi wa shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) — kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye soka la Afrika hasa kifedha pamoja na kiufundi pia.
Kabla ya Patrice Motsepe kuchaguliwa kuwa raisi wa shirikisho mwaka 2021, CAF ilikuwa inakabiliwa na madeni makubwa yaliyofikia hadi $140 million (TSH 360 billion).
Lakini chini ya uongozi wake CAF ilitangaza kupata faida ya $9.5 million (TSH 24 billion) Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 8 kupita — huku mapato ya kila mwaka yakiongezeka hadi kufikia $150 million (TSH 387 billion) kutokana na mikataba ya TV rights na udhamini.
Patrice Motsepe chini ya uongozi wake ameweza kuleta ushindani na thamani kubwa kwenye mashindano yote hapa Afrika na ni baada ya kuongeza kwa kiasi kikubwa zawadi za washindi kwa mashindano yote.
Bingwa wa AFCON hivi sasa anapokea $7 million (TSH 18 billion) — ikiwa ni ongezeko la asilimia 40% kutoka kwenye zawadi ya hapo awali na inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia $10 million hivi karibuni.
Kwa upande wa WAFCON zawadi imeongezeka kwa asilimia 45%, ambapo bingwa kwa sasa anapokea $1 million (TSH 2.5 billion).
Uongozi wa Patrice Motsepe pia umeweza kuongeza ruzuku kwa upande wa vilabu, ambapo kwa sasa kila klabu inayoshiriki CAFCL na CAFCC hatua ya awali inapewa $100k (TSH 258 million) kwa ajili ya kusaidia gharama za usafiri.
Haya niliyoyazungumzia hapa ni mafanikio ya upande wa kifedha tuu (financial) — lakini bado kuna mafanikio mengine kwenye kila nyanja kwenye wakati wake ndani ya CAF.
Huyu ni moja ya viongozi bora zaidi waliowahi kuliongoza hili shirikisho toka lilipoanzishwa rasmi — ndio kwanza anamiaka 4 tuu, lakini mabadiliko ni makubwa mno.✍️

Comments