Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema mwamuzi yeyote atakayeharibu mchezo wa kesho wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba, watamfungia maisha kujihusisha na mpira wa miguu.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa TFF unaofanyika hapa Kahama, Karia, amesema mbali na kumfungia maisha pia watamfungulia mashataka.
"Naomba niseme hapa kwenye mkutano mkuu na waamuzi wanisikie, atakayeharibu mchezo wa kesho hatutamuacha salama, malalamiko yamekuwa mengi na yanaharibu taswira ya mchezo," amesema Karia.

Comments