NMB YATOA ZAIDI SH. BIL. 12 KWA WAFANYABIASHARA 6,011

Jumla ya Sh.12.4 bilioni zimeshatolewa na Benki ya NMB kwa zaidi ya wafanyabiashara 6,011 ambapo wanufaika wamepewa Elimu ya fedha na uongozi.

 

Takwimu hizo zimetolewa na Meneja Mwandamizi idara ya Biashara za Serikali Amanda Feruzi kwenye mkutano wa Jumuiya ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Ukanda wa Ziwa Victoria (LVRLAC) unaoendelea kwenye Ukumbi wa Jiji la Dodoma.

 

Fedha hizo ni kati ya Sh13 bilioni ambazo Serikali ilizitoa kwa NMB kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vijana, Wanawake na wenye ulemavu katika mfumo wa majaribio kwa Halmashauri 6.

 

Halmashauri zilizochaguliwa kwa mfumo wa majaribio ni Majiji ya Dar es Salaam na Dodoma, Manispaa ya Songea, Halmashauri za Newala, Bumbuli na Itilima.

 

Feruzi amesema NMB ipo tayari kufanya kazi na Jumuiya hiyo kama ambavyo imekuwa na ushirikiano na kufadhiri mikutano yao kila mwaka.

 

Amesema benki imekuwa na ushirikiano na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya uwezeshaji wananchi kupitia fedha zinazotengwa kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na wenye ulemavu.

 

"Benki ya NMB ina ujuzi na uzoefu katika APF kwani imeweza kutoa hati fungani zake na Taasisi nyingine zenye thamani ya Trilioni Moja ikiwa benki ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kutoa hati fungani ya Jinsia (Jasiri Bond) na Uendelevu (Jamii Bond),ambazo zimevutia wawekezaji wa ndani na nje katika masoko ya mitaji ya Kimataifa," amesema Feruzi.

 

Kwa mujibu wa maalumu hiyo, NMB ilikuwa benki ya kwanza kuunganishwa katika mfumo wa GePG ambako kazi kubwa ilifanyika katika ukusanyaji wa mapato ambayo ilitokana na Uwekezaji mkubwa katika Teknolojia, bidhaa na huduma mbalimbali hata kuifanya kuwa mstari wa mbele katika kubuni masukuhisho kwa wateja na Serikali.

 

Akizungumza mkutano huo ambayo uliwakusanya wajumbe 42 kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera, Feruzi amewataka kutumia fursa iliyotolewa na Serikali ya kutafuta mitaji kutoka kwa wawekezaji ili kuzalisha vyanzo vipya vya mapato.

 

"Benki inaishauri Serikali kupanua wigo wa kutafuta fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati kwa kushirikiana na Sekta binafsi kupitia uwekezaji kwa njia ya PPP na APF," amesema Feruzi.

 

Ametaja baadhi ya manufaa yatakayopatikana kupitia uwekezaji huo ni kutatua na kusaidia maboresho ya Miundombinu kwa haraka, kupunguza utegemezi kwenye bajeti Kuu, kuruhusu utekelezaji wa miradi mara moja na kushirikiana na kutumia uzoefu wa Sekta binafsi katika kutafuta mitaji.

 

Akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Reuben Kwagilwa, amewataka Wakurugenzi kote nchini kufanya kazi kwa mashirikiano na Sekta binafsi huku akisisitiza kuitumia benki ya NMB katika masuluhisho ya kifedha.

 

Naibu Waziri amesema maeneo mengi kumekuwa na kulegalega katika matumizi ya fedha jambo alilosema Serikali haitamvumilia mtumishi atakayebainika.

 

"Nanyi Wakurugenzi niwaagize kwamba mlipe madeni ya Jumuiya kwa wakati ili kusudi muweze kujiendesha na mnaweza kufanikiwa mkishirikiana na NMB katika Mipango yenu," amesema Kwagilwa.

 

Katika hatua nyingine Naibu Waziri amewataka Wakurugenzi kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua badala ya kusubiri viongozi wa juu kuja kuwasikiliza wananchi.





Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Reuben Kwagilwa (kushoto) akisalimiana na Meneja mwandamizi wa biashara za serikali na benki ya NMB ,Amanda Feruzi wakati alipowasili kufungua mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya mamlaka za serikali za mitaa ukanda wa ziwa victoria uliofanyika Jijini Dodoma, NMB ni mdhamini mkuu wa mkutano huo.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

MAJESHI YA URUSI CHINA NA IRANI YAANZA MAZOEZI YA PAMOJA DHIDI YA MAREKANI

PUNGUZA STRESS....