Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
Katika kipindi chote cha utumishi wake, Kardinali Pengo alisimama imara katika kuhubiri amani, maadili na mshikamano wa kitaifa. Alikuwa sauti ya busara katika masuala ya kijamii na kimaadili, akihimiza amani, heshima na utu katika jamii yetu. Mchango wake katika malezi ya kiroho na maendeleo utaendelea kukumbukwa na kuenziwa siku zote.
Ninatoa pole kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, Maaskofu, Mapadri, Watawa, familia, ndugu, jamaa, marafiki, waumini wa Kanisa Katoliki na Watanzania wote kwa msiba huu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Amina.

Comments