TCRA YATOA AHUENI KWA WAENDESHA MAUDHUI MITANDAONI

Na Richard Mwaikenda, Dodoma

Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa nafuu ya kutolipa ada ya mwaka mmoja kwa waandishi wa habari wanaoanzisha mitandao ya habari kwa mara ya kwanza ambapo imeelezwa kuwa watajulikana kama 'Amateur'.


Nafuu hiyo, imetengazwa na Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,Mhandisi Andrew Kisaka alipokuwa akiwasilisha matokeo na utekelezaji wa mapendekezo yatokayo na utafiti wa huduma za utangazaji nchini katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Februari 12, 2026 jijini Dodoma.


Mhandisi Kisaka amesema kuwa wametoa nafuu hiyo ili kuwapa muda waandishi wa habari wa kujifunza na kupata uzoefu wa uendeshaji wa mitandao ya habari. 


Awali anayetaka kuanzisha mtandao wa habari alitakiwa alipe ada ya maombi Sh. 50,000 na ada ya leseni sh. 500,000 kwa mwaka.


Hatua hiyo, imepokelewa kwa furaha na wamiliki wa mitandao waliohudhuria mkutano huo ambao baada Mhandisi Kisaka kutangaza walipiga makofi. 


Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku mbili ni wanachama wa Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN), Jumuiya ya  Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), MOAT, NIBA, Wakongwe RTD, Baraza la Habari Tanzania (MCT), MISA Tanzania na EACO.

Kwa niaba ya Waziriu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, mkutano huo umefunguliwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamisi Mwinjuma.


Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA,Mhandisi Andrew Kisaka.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam SJMC-UDSM, Zuhura Selemani.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo.











Kikundi cha ngoma cha Nyati kikitumbuiza katika mkutano huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

Wasifu wa Kizza Besigye

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

CCM YAMJIBU BUTIKU CHADEMA KUFUNGIWA