JOPO LA WATALAAMU KWENDA MIKOANI KUHAKIKI VIJANA WANAOTARAJIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT YA KUJITOLEA
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema timu ya wataalam kutoka Makao Makuu ya JKT iko tayari kwenda katika Mikoa yote Tanzania ili kufanya uhakiki wa vijana wanaotarajiwa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa kujitolea.
Brigedia Jenerali Mabena ameyasema hayo leo tarehe 17 Februari 2026 muda mfupi baada ya kufungua Semina Elekezi kwa Maafisa waandikishaji wa vijana wa kujitolea 2026 kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele iliyofanyika katika ukumbia wa Mabele uliopo Jijini Dodoma.
Aidha, Brigedia Jenerali Mabena ameongeza kuwa timu hiyo inayojumuisha wataalam mbalimbali ni miongoni mwa Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma ambao wamekula kiapo cha Utii na Uaminifu wapo tayari kutekeleza jukumu hilo.
Itakumbukwa Januari 20, 2026 Jeshi la Kujenga Taifa kupitia vyombo vya Habari lilitoa wito wa Vijana wote toka Tanzania Bara na Visiwani kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea.

Comments