Timu ya Young Africans SC (Yanga) imemteua Mhandisi Ghalib Said Mohamed, Mwenyekiti wa GSM Group, kuwa mwekezaji na mkandarasi mkuu wa ujenzi wa uwanja wao mpya.
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB:
Klabu ya Young Africans Sports Club (YANGA SC) kwa udhamini wa GSM Group inapanga kujenga uwanja wa kisasa wa kiwango cha juu kimataifa, unaokidhi viwango vya FIFA na Confederation of African Football (CAF).
Sifa Kuu za Uwanja:
Pitch ya kisasa yenye vipimo rasmi (105 x 68), nyasi bora, mifumo ya umwagiliaji na uondoshaji maji wa kisasa.
Taa za kimataifa (1600–2000+ lux) zinazowezesha matangazo ya 4K pamoja na umeme wa akiba.
Uwezo wa mashabiki 30,000–80,000+, ukiwa na sehemu za VIP, VVIP na hospitality suites.
Teknolojia ya kisasa ikiwemo VAR rom, skrini kubwa, na CCTV.
Miundombinu kamili ya wachezaji, waamuzi na vyombo vya habari, pamoja na huduma za afya na usalama wa hali ya juu.
Mradi huu unalenga kuiweka YANGA SC katika ramani ya soka la dunia na kuimarisha maendeleo ya michezo nchini.

Comments