WILAYA YA RUNGWE NA WABUNGE WAKE.


Wilaya ya Rungwe ni moja ya wilaya zinazounda Mkoa wa Mbeya. Wilaya hii imepakana na Wilaya ya Mbeya kwa upande wa Kaskazini, kwa upande wa Mashariki inapakana na Mkoa wa Njombe, kwa upande wa Kusini-mashariki inapakana na Wilaya ya Kyela, upande wa Kusini-magharibi inapakana na Wilaya ya Ileje.

Jina la Rungwe limetokana hasa na kituo cha Misioni ya Kanisa la Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya Mlima Rungwe (Mlima wa tatu kwa urefu Tanzania). Hiki kituo cha Rungwe Mision kipo takribani kilomita 20 kutoka Mji wa Tukuyu, mji (Tukuyu) ambayo ndiyo Makao makuu ya Wilaya ya Rungwe.

Wilaya Rungwe inaundwa na Halmashauri mbili. Hizi ni Halmashauri mbili zilizigawawanywa mwaka 2013 baada ya kutenga Kata 11 kutoka Halmashauri ya Rungwe na kuunda Halmashauri mpya ya Busokelo. 

Kwa kifupi niseme Wilaya ya Rungwe kwasasa inazo Halmashauri mbili za Rungwe na Busokelo, na pia wilaya hii ina takribani jumla ya Kata 42 ambazo ni pamoja na Bagamoyo, Bujela, Bulyaga, Ibighi, Ikama, Ikuti, Ilima, Isange, Itete, Kabula, Kambasegela, Kandete, Kawetele, Kikole, Kinyala, Kisegese, Kisiba, Kisondela, Kiwira, Kyimo, Lufingo, Lufilyo, Lupata, Luteba, Lwangwa, Makandana, Malindo, Masebe, Masoko, Masukulu, Mpombo, Mpuguso, Msasani, Ndanto, Nkunga, Suma, Swaya na kadhalika.

Majina ya wabunge wa Rungwe tangu Uhuru ni: Jeremia Kasambala (1961- 65), Exson Mbembela (1965 - 70), Joel Mwambola (1970 - 75), John Mwakangale (1975 - 80), Esiri Mwakyambiki (1980 - 85), Emmanuel Mwambulukutu (1985 - 2000), David Mwakyusa (2000 - 2015), Saul Henry Amon (2015 - 2020) na Anthony Mwantona (2000 - hadi sasa)

Na kwa upande wa Jimbo la Busokelo (Rungwe-mashariki) ambalo nalo liko ndani ya Wilaya ya Rungwe, wabunge wake tangu Uhuru ni: Elly Anangisye Mwalulesa (1965 - 69), Joel Mwambola (1969 - 70), mwaka 1970 Jimbo la Busokelo likafutwa na likaja kurejeshwa mwaka 1995 ambapo Ambangile Ndepania akachaguliwa kuwa Mbunge. Ambangile Ndepania (1995 - 2000), Mark Mwandosya (2000 - 2015) na Atupele Mwakibete (2015 -2025) na Lutengano Mwalwiba (2025 - hadi 
sasa).

Ningekupa nafasi ya kumwelezea Mbunge mmoja kati ya wabunge wote niliowataja, ni Mbunge yupi unaweza kumwelezea vizuri?

Lusako Mwang'onda  
Kisasa, Dodoma.
19 Februari, 2025.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO