DKT.MIGIRO AIMARISHA USHIRIKIANO KIMATAIFA NA MABALOZI WA CUBA, VIETNAM, NA UN

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi, Dkt. Asha-Rose Migiro, kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo ya makao makuu  CCM, Lumumba, jijini Dar es salaam.
Mabalozi hao ni Mheshimiwa Yordenis Despaigne Vera, Balozi wa Jamhuri ya Cuba na Mheshimiwa Vu Thanh Huyen, Balozi wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, wote wenye makaazi yao nchini Tanzania.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya CCM na vyama rafiki vya CPC–Cuba na CPV–Viet Nam, hususan katika maeneo ya uongozi, mshikamano wa vyama vya siasa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Migiro, alifanya mazungumzo na Mheshimiwa Susan Ngongi Namondo, Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, ambapo walijadiliana vipaumbele vya maendeleo ya jamii katika utekelezaji wa baadhi ya maeneo yaliyomo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 ambayo yanawiana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,  na Malengo ya Maendeleo ya Kimataifa (SDGs).









 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

TANZIA;.KWA KHERI DADA YETU MPENDWA EDITHA, TASNIA IMEPATA PIGO

NATAKA TANZANIA, KENYE NA UGANDA IWE NCHI MOJA, ILI BAHARI YA HINDI IWE YETU SOTE - MUEVENI

RAIS SAMIA AWASILI IRINGA KWENDA MEI MOSI NJOMBE

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA