MAKAMU MWENYEKITI UWT ZAINAB SHOMARI AWAPONGEZA WANAWAKE KUICHAGUA CCM, ASISITIZA UTEKELEZAJI THABITI WA ILANI YA 2025–2030

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Mhe. Zainab Khamis Shomari (MNEC) amewapongeza wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa mshikamano mkubwa waliouonesha wakati wa kampeni na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.


Mhe. Zainab amesema wanawake wameendelea kuwa nguzo muhimu ya ushindi wa CCM kutokana na kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli mbalimbali za kampeni, kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura pamoja na kuendelea kukiamini chama hicho kutokana na utekelezaji wa sera zake zinazolenga kuwaletea wananchi maendeleo.

Amesema ushindi huo ni matokeo ya imani kubwa waliyonayo wananchi kwa CCM chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kusimamia kwa vitendo agenda ya maendeleo, ustawi wa wanawake, vijana na makundi mbalimbali ya kijamii nchini.

Makamu Mwenyekiti huyo wa UWT ameeleza kuwa nguvu na mchango mkubwa uliotolewa na wanawake katika kuhakikisha CCM inapata ushindi hautapotea bure, bali utalipwa kupitia utekelezaji madhubuti wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 ambayo imebeba vipaumbele mbalimbali vya maendeleo kwa wananchi wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla.

“Wanawake mmefanya kazi kubwa sana kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo. Chama na Serikali vinatambua mchango wenu, na sasa jukumu letu ni kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa kikamilifu kwa manufaa ya wananchi wote,” amesema Mhe. Zainab.

Ameongeza kuwa Serikali ya CCM tayari imeanza utekelezaji wa Ilani hiyo mara baada ya kuapishwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa katika sekta za afya, elimu, maji, miundombinu, uwezeshaji wa wanawake na vijana pamoja na kukuza uchumi wa wananchi.

Mhe. Zainab ametoa rai kwa wanawake kuendelea kuwa wamoja, kuilinda CCM na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ili kuendelea kudumisha mafanikio yaliyopatikana chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema hayo leo Aprili 30, 2026 katika Kongamano la kuwashukuru Viongozi wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha ushindi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025

#UWTimara
#UWTjeshilaDktSamiaNaDktMwinyi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#KongamanolaUWTdsm





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

AINA 10 ZA WANAWAKE AMBAO BIBLIA INAKUONYA UWAEPUKE

MAJANI YA MAPERA NA MATUMIZI YAKE YA KITIBA

RAIS ALİYEISHI KAMA MUNGU WAKATI WATU WAKE WAKIFA NJAA

ZIJUE TIBA ZA MMEA WA MSHONA NGUO.