WENGER AIPONGEZA SERENGETI BOYS

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka Duniani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) na kocha wa zamani wa Arsenal, Arsène Wenger, amevutiwa na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys), kufuatia mchezo wao mgumu wa hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Misri.

​Katika video maalum aliyoituma, nguli huyo wa soka ametoa pongezi za dhati kwa vijana hao kwa niaba ya FIFA, akivutiwa na soka safi, la kisasa na la ushindani wa hali ya juu walilolionyesha dimbani kwenye hatua hiyo kubwa na yenye presha kubwa ya nusu fainali dhidi ya miamba hiyo ya Kaskazini mwa Afrika.

​"Mlicheza vizuri sana, na nawapongeza kwa niaba ya FIFA kwa sababu mlicheza soka safi sana la kuvutia, na Misri nao walicheza vizuri pia. Mlikuwa na mchezo mzuri na mwisho wa siku tulishuhudia mechi ya ushindani na ya kupendeza sana. Natumai tutaonana tena hivi karibuni, na tuonane pia kwenye..."

​Pongezi hizi kutoka kwa mmoja wa wataalamu wakubwa wa soka duniani kwenye hatua hii ya nusu fainali ni kielelezo tosha kuwa uwekezaji unaofanywa katika soka la vijana nchini umeanza kuonekana na kugusa rada za FIFA, jambo linalotoa matumaini makubwa kwa vijana wetu kuelekea fainali na mustakabali mzima wa soka la Tanzania. #NestoShayoUPDATES



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

TANZIA;.KWA KHERI DADA YETU MPENDWA EDITHA, TASNIA IMEPATA PIGO

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

RAIS SAMIA AWASILI IRINGA KWENDA MEI MOSI NJOMBE

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI