DK MAGUFULI AZURU KABURI LA NYERERE, AKABIDHIWA KIFIMBO CHA NYERERE

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akizuru kaburi la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo, wilayani Butiama, Mkoa wa Mara jana , aliposimama kwa muda akielekea kwenye mkutano wa kampeni wilayani huo leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli akiweka shada la la maua alipozuru kaburi la Baba wa Taifa marehemu Julius Nyerere, katika Kijiji cha Mwitongo wilayani Butiama, Mkoa wa Mara, aliposimama kwa muda akienda kufanya mkutano wa kampeni wilayani huo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Msanii Dokii na Mwakilishi wa watu wenye ulemavu Aman Mpanju wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi hilo
 Dk Magufuli akiwasha mishumaa alipozuru kaburi hilo leo
 Dk Magufuli, Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba, wasanii na  viongozi wengine wakiwa na mashada ya maua wakijiandaa kuweka kweenye kaburi hilo
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Butiama leo

 Baadhi ya wananchi wakiwa wamejikinga na kwa kutumia bendera wakati wa mkutano huo
 Dk Magufuli akiwanadi wagombea ubunge; Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) wa Jimbo la Musoma Vijijini na Nimrod Mkono wa Jimbo la Butiama
 Wananchi wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli alipokuwa akihutubia na kujinadi katika mkutano huo wa kampeni mjini Butiama
 Profesa Muhongo akikabidhiwa Ilani ya Uchaguzi na Dk Magufuli. Pia Mkono naye alikabidhiwa Ilani hiyo
 Mgombea urais wa Ta nzania kupitia CCM, John Magufuli akikwasalimia wananchi huku akiwa na kifimbo alichozawadiwa na Wazee wa Kimila wa Kabla la Wazanaki wakati wa mkutano wkampeni wilayani Butiama alioufanya baada ya kuzuru kabila la marehemuBBaba wa Taifa  Mwalimu Julius Nyerere Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli  akimuonesha  Waziri Mkuu wa zamani, Jaji mstaafu Joseph Warioba kifimbo alichokabidhiwa zawadi na na Wazee wa Kimila wa Kabla la Wazanaki wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Butiama alioufanya baada ya kuzuru kabila la marehemuBBaba wa Taifa  Mwalimu Julius Nyerere Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo jana. Kulia ni Mjumbe wa  kamati ya kampeni za CC
 Dk Magufuli akiwasili kuanza kampeni katika mkoa wa Mara baada ya kumaliza katika Mkowa wa Tanga
 Dk Magufuli akimsalimia mtu mwenye ulemavualipowasili
 Dk Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ShyRose Bhanji wakati wa mapokezi
 Chifu wa Wazanaki, Japhet Wanzagi akisalimiana na Dk Magufuli. Kulia ni Makongoro Nyerere
Dk Magufuli akikabidhiwa zawadi ya Kifimbo cha Mwalimu Nyerere wakati wa mkutano huo wa kampeni wilayani Butiama

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO