FEDHA ZA UVIKO 19/IMF SH. MIL. 470 ZAOKOA UJENZI WA SEKONDARI PEKEE KATA YA IFULIFU, MUSOMA VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa na VIONGOZI wa ujenzi wa Ifulifu Sekondari ya Kata ya Ifulifu aliofanya nao kikao katika Kijijini cha Kabegi, eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kata.


WANAKIJIJI wa Kata ya Ifulifu wamezipokea kwa furaha fedha za UVIKO 19/IMF sh. mil. 470 kusaidia ukamilishaji ujenzi wa shule pekee ya sekondari katika kata hiyo.


Kata ya IFULIFU inayojenga Sekondari yake ya Kata tokea JUNI 2017, imepokea kwa shukrani nyingi mno SHILINGI MILIONI 470 kutoka Serikali Kuu.


Wanavijiji na viongozi wa Kata ya Ifulifu wametoa shukrani nyingi sana kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimbuka Kata yao ambayo haina Sekondari, na ujenzi wake ulikuwa unasuasua kwa ukosefu wa fedha.


Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, hivi karibuni alienda Kijijini Kabegi kufuatilia ujenzi wa Ifulifu Sekondari na kujadili na Viongozi wa Kata hiyo kuhusu matumizi bora ya TSH MILIONI 470 walizozipokea kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.


Prof. Muhongo alitoa ushauri kuwa vijiji 2 vya Kabegi na Kiemba vifanye VIKAO vya WANAVIJIJI kuwaeleza juu ya malengo ya fedha hizo (Tsh 470m) walizozipokea kutoka Katani na kwamba matumizi yake yawekwe wazi kwa wanakijiji..


Pia, amewataka wanavijiji kuendelea  kuchangia nguvukazi ili miundombinu muhimu ya elimu ipatikane kutokana na fedha hizo. Ujenzi uende kwa kasi kubwa na kwa ubora unaokubalika.


*Ifulifu Sekondari ifunguliwe Julai 2022., na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na kutoka Vijiji vya Kabegi na Kiemba waendelee na masomo yao kwenye Sekondari yao ya Kata.


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI