“Mimi napenda sana pilau, ndiyo chakula changu pendwa, makange ya samaki napenda sana, chapati, chipsi mayai, hivyo ndivyo vyakula ambavyo hapa Tanzania navipenda sana, lakini ugali hapana sipendi wala wali sio mpenzi sana, unajua mimi sio mtu mlaji sana na bahati mbaya sipendi kula chakula ambacho sikifahamu lakini namshukuru mke wangu anaendelea kunibadilisha taratibu.
.
“Namshukuru Mungu nina mke ambaye anaelewa ni mambo gani natakiwa kuzingatia wakati wa vyakula, unajua maisha yetu muda mrefu tunakuwa kambini, ni siku chache sana tunakuwa nyumbani
.
“Lakini mke wangu anazingatia sana vyakula ambavyo sitakiwi kuvitumia san ili nisiongeze uzito wa mwili na wakati mwingine namsaidia kumwelewesha hiki sitakiwi kufanya sasa wala kukitumia na anaelewa.“ — Aziz Ki. [Mwanaspoti]

Comments