NMB TELEZA KIDIGITALI NDANI YA A-TOWN

 

Kwa mara nyingine tena, Benki ya NMB katika kuendeleza ubunifu na kuwarahisishia huduma wateja wake, inaendelea kuinadi kampeni ya Teleza Kidijitali iliyozinduliwa May 09, 2022 na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Ruth Zaipuna, katika soko la Tandika jijini Dar es Salaam kwa kuingia mtaani na kuwaelimisha Watanzania umuhimu wa huduma zilizo chini ya kampeni hio, ambazo ni NMB Pesa Wakala, Lipa Mkononi na Mshiko Fasta.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, NMB ilifikisha kampeni hiyo jijini Arusha, ambapo lengo kuu ni kusogeza huduma kwa wananchi ili waweze kutumia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo nafuu.

Akizundua kampeni hio katika Soko la Kilombero jijini Arusha, Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, alisema kampeni hio imelenga kutoa elimu ya kutosha na kuwaingiza Watanzania wengi zaidi kwenye Sekta rasmi ya kibenki ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali ambazo wanazitoa.

Lakini pia, aliwasisitizia kuchangamkia fursa ya Mshiko Fasta ambapo mteja anaweza kupata mikopo nafuu isiyo na dhamana kupitia simu yake tu ukiwa na NMB Mkononi. 

Aidha, Mponzi aliongezea kuwa wale wenye sehemu zao za biashara, Benki ya NMB inatoa huduma ya Lipa Mkononi, ambayo inamuwezesha mfanyabiashara au mjasiriamali kulipwa pesa za mauzo moja kwa moja katika akaunti yake kiurahisi na kwa usalama bila kulazimika kuhamisha fedha nyingi kutoka eneo lake la biashara kwenda tawini.

“Pia, NMB Pesa Wakala, ni huduma inayomuwezesha mtu yeyote kuwa wakala kwa kupitia simu yako ya mkononi (smart phone au tochi) kutoa huduma za kuweka, kutoa au kutuma pesa kiurahisi,” alisema Mponzi.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Kilombero wameishukuru NMB kwa kuwaletea huduma hiyo itakayowasaidia kupata mikopo ya fedha kwa ajili ya kujiinua kichumi.

“NMB wametuletea njia rahisi ya kufanya biashara, kwa sababu wapo baadhi ya wateja wanataka kununua kwa njia ya kibenki, hii itaturahisishia hata hatutakuwa na haja ya kutafuta chenji. Vilevile fedha zetu za mauzo zitakuwa salama hatutakuwa na haja ya kusafirisha fedha nyingi kuzipeleka benki,” alisema Hassan Athumani.

Mwisho

Pic 1: Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi akizindua kampeni ya Teleza kidijitali, iliyofanyika kwenye Soko la Kilombero jijini Arusha.

Pic 2: Wateja wakifungua akaunti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Teleza kidijitali, iliyofanyika Soko la Kilombero jijini Arusha.

Pic 3: Baadhi ya wakazi wa Arusha waliohudhuria kwenye kampeni ya Teleza Kidijitali iliyozinduliwa kwenye Soko la Kilombero jijini Arusha.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

KAMONGA AIOMBA SERIKALI KUIPA KIPAUMBELE LUDEWA UWEKAJI UMEME KWENYE VITONGOJI+video

UTAFITI WAJA NA 'DAWA MPYA' YA KUSAIDIA TIBA YA WAGONJWA WA AFYA YA AKILI +video

SILLO AISHAURI SERIKALI KUIWEZESHA TRA IWE NA MIFUMO MIZURI YA UKUSANYAJI KODI+video

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

BUTONDO:TUNAOMBA AMBULANCE IKASAIDIE TARAFA YA MONDO KISHAPU+video

Xi REPLIES TO LETTER FROM CARDRE WORKSHOP PARTICIPANTS AT NYERERE LEADERSHIP SCHOOL

SERIKALI YAAHIDI KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI KISHAPU

SHULE YA PAMOJA YA ARUMERU WAFUNDISHWA BUNGENI UHUSIANO WA BUNGE NA RAIS, UMUHIMU WA SIWA+video