TANZANIA NA JAPAN KUSHIRIKIANA UKUZAJI UJUZI KWA VIJANA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Utalii wa Japan Mhe. Kenichi Ogasawara kuhusu kuimarisha ushirikiano katika masuala ya ukuzaji ujuzi na teknolojia kwa vijana.

Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo Machi 21, 2025 Jijini Dodoma alipokutana na ujumbe kutoka nchini Japan.

Aidha, amesema kupitia programu ya ukuzaji ujuzi inayotarajiwa kuanzishwa baina ya nchi hizo mbili italeta tija kwa vijana kuweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi watakaoupata kutoka nchini Japan.

Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. DKt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufungua mipaka nje ya nchi ili kutoa fursa kwa watanzania kupata kazi nje ya nchi.

Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Utalii wa Japan Mhe. Kenichi Ogasawara amesema kuwa Tanzania ni moja ya Nchi ya kipaombele katika program hiyo ya mashirikiano ya ukuzaji ujuzi na teknolojia kwa vijana wa Kitanzania.







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE