Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa, Mary Chatanda (kushoto) akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mmbaga wakishiriki kumuombea dua maalumu Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Iftar iliyoandaliwa na UWT katika msikiti wa Gaddaf jijijni Dodoma Machi 29, 2025.
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Alhaj Mustafa Rajabu Shaban ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT), kwa kuwaandalia iftar ya kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Msikiti wa Gaddaf jijini Dodoma.
Sheikh amesema kuwa ni haki Rais Samia kumuombea dua kwani hata yeye kwa utafiti wake amegundua kwamba ni kiongozi anayeongoza kwa kuombewa duwa za siri na za hadharani kwani anawafanyia mema watanzania jambo ambalo hata Mungu anapenda.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa UWT Taifa na wa mkoa huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, viongozi na waumini wa msikiti huo wakiongozwa na sheikh huyo, Jumuiya mbalimbali za kiislamu pamoja na makundi ya watu wenye uhitaji.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda,amewaomba Watanzania ifikapo Oktoba wakati wa Uchaguzi Mkuu wasipoteze muda kuwapigia kura ya urais wagombea wanaume wa chama chochote, bali kura zote wampigie Dkt. Samia Suluhu Hassan wa CCM.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa, Mary Chatanda (kushoto) akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mmbaga pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (kulia).
Waumini wa Kiislamu wakishiriki kuomba dua hiyo.
Wakipata futari
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments