*
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amefanya mkutano Kijijini Bugoji.
*Lengo la Mkutano:*
(i) kusikiliza na kutatua kero za wanavijiji
(ii) kueleza fursa za uchumi zilizopo kwa wakati huu na ujao
(iii) kutanzua mikwamo ya utekelezaji wa miradi ya vijiji vitatu vya Kata ya Bugoji
*Fursa za Uchumi zilizoelezwa kwa kirefu na Mbunge huyo:*
*Mikopo ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kutoka Benki za CRDB, NMB na NBC
*Kilimo cha Umwagiliaji kwenye Bonde jirani la Bugwema.
*Miradi midogo midogo ya umwagiliaji kwa kutumia maji ya visima
*Uvuvi wa vizimba ndani ya Kata 18 (kati ya Kata 21 za Jimboni mwetu) zilizoko pembezoni mwa Ziwa Victoria
*Mikopo nafuu ya kutoka Halmashauri yetu, yaani kutoka kwenye 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri yetu
*Miradi inayohitaji kuongezewa kasi ya utekelezaji:*
1. Kijiji cha Bugoji: Dan Mapigano Sekondari
*Sekondari ina maabara moja ya somo la baiolojia. Misingi ya ujenzi wa maabara nyingine mbili (fizikia & kemia) ipo lakini ujenzi umesimama kwa muda mrefu!
*Uamuzi: ujenzi wa maabara 2 za masomo ya sayansi uendelee
*Saruji Mifuko 100: Mbunge wa Jimbo atachangia saruji hiyo iwapo ujenzi wa maabara hizo mbili utaendelea.
2. Kijiji cha Kaburabura: Zahanati ya Kijiji
*Kijiji kimeamua kujenga Zahanati yake. Harambee ya ujenzi ilishapigwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini
*Ujenzi umesimama baada ya Kijiji kupokea fedha (Tsh 88.6m) kutoka Serikalini za kujenga Shule Shikizi Kaburabura iliyoko Kitongoji cha Songambele
*Uamuzi: Mkutano wa Kijiji uitishwe kesho kujadili mwendelezo wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao
*Saruji Mifuko 200: Mbunge wa Jimbo alishachangia saruji mifuko 50 kati ya 200 ya ahadi yake. Ujenzi ukiendelea Mbunge huyo nae ataendelea kuchangia
3. Kijiji cha Kanderema
*Wanakijiji wameamua kujenga sekondari yao.
*Eneo la ujenzi limepatikana na Serikali ya Kijiji inafanya mawasiliano ya kupata kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri yetu.
*Saruji Mifuko 100. Kijiji kikianza ujenzi Mbunge wa Jimbo atawachangia saruji hiyo, na ataenda kijijini hapo kupiga Harambee ya ujenzi
*MICHANGO INAKARIBISHWA*
Wadau wa Maendeleo ya Musoma Vijijini wakiwemo Wazaliwa wa vijijini mwetu wanakaribishwa kuchangia miradi hiyo iliyoelezwa hapo juu. Michango itumwe moja kwa moja kwa kijiji husika.
Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:
Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo na Wanavijiji wa Kata ya Bugoji. Mkutano ulifanyika leo Kijijini Bugoji
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatano, 2 April 2025
Comments