MKUTANO MKUU WA WANAUME KUFANYIKA DODOMA

Umoja wa Wanaume Tanzania unatarajia kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi huu wa nne na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa umoja huo utakaofanyika Dodoma.

Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amesema hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, wakati DC Gondwe alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, kufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanaume Tanzania, ambao umefanyika Mkoani Singida ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkubwa utakaofanyika Mkoani Dodoma utakaombatana na uzinduzi wa umoja huo.

DC Gondwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, ametoa wito kwa Umoja wa Wanaume Tanzania kuwa chachu ya maadili mema kwa Vijana wa kiume na akina Baba “Tumieni Umoja huu, kuwakumbusha Vijana wa kiume na akina Baba, kuwajibika katika Familia  na nchi ili kupunguza madhara yanayotokea kwa kuharibi familia, katika tamaduni zetu, Wamasai wana njia bora ya kulea Vijana wa kiume kuwa Wanaume, zipo tamaduni zetu bora zitunzwe"

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amekabidhi Katiba ya Umoja na Nyaraka mbalimbali za Usajili naGondwe ameahidi kuzifikisha kwa Mkuu wa Mkoa Halima Dendego ambaye amewaahidi kuwapa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Wanaume Tanzania.

Malengo makuu ya umoja huo ni kuwaunganisha Wanaume wote ndani ya Tanzania na kuwa kitu kimoja ili washirikiane kupinga kwa nguvu zote aina zote za ukatili ndani ya Jamii hususani ni kwa Wanawake na Watoto na hata baadhi ya Wanaume wanaonyanyaswa kuanzia ngazi ya Familia na Jamii. #MillardAyoUPDATES



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE

#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA MJI WA KIHISTORIA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO

HUU NDIO UKWELI ULIVYO RAFIKI YANGU

BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA