Timu ya Taifa (Tanzania) ya Kriketi chini ya miaka 19 imefuzu fainali za Kombe la Dunia kwenye mchezo wa Kriketi baada ya leo kuibuka washindi dhidi ya Sierra Leone.
Ushindi wa leo dhidi ya Sierra Leone umeipa ubingwa Tanzania katika michuano ya Kufuzu Kombe la Dunia Kriketi ambayo imefanyika jijini Lagos, Nigeria.
Fainali za Kombe la Dunia za mchezo huo zitafanyika mwakani (2026 ICC U19 Men’s World Cup).
Comments